Biblia inasema nini kuhusu Ulafi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ulafi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ulafi

Kutoka 16 : 21
21 Basi wakaokota asubuhi baada ya asubuhi, kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa; na hapo jua lilipokuwa ni kali, kikayeyuka.

Kutoka 16 : 27
27 Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione.

Hesabu 11 : 33
33 Kisha hapo hiyo nyama ilipokuwa ikali kati ya meno yao, hawajaitafuna bado, hasira za BWANA ziliwaka juu ya watu, BWANA akawapiga watu kwa pigo kuu mno.

Kumbukumbu la Torati 21 : 21
21 ⑬ Wanaume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.

Mithali 23 : 21
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.

Mithali 30 : 22
22 Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula;

Mhubiri 10 : 17
17 Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.

Isaya 22 : 13
13 na kumbe! Furaha, na kuchekelea, na kuchinja ng’ombe, na kuchinja kondoo, na kula nyama, na kunywa mvinyo; tule, tunywe, kwa maana kesho tutakufa.

Amosi 6 : 7
7 Basi kwa ajili ya hayo sasa watakwenda utumwani pamoja na wa kwanza watakaokwenda utumwani, na kelele za shangwe za hao waliojinyosha zitakoma.

Luka 12 : 20
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?

Luka 12 : 46
46 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini.

Luka 21 : 34
34 Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;

Warumi 13 : 14
14 ⑩ Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.

1 Wakorintho 15 : 32
32 Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nilipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa.

Wafilipi 3 : 19
19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao uko katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.

1 Petro 4 : 3
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuishi katika uzinzi, tamaa, ulevi, na karamu za kula na kunywa vileo kupindukia, na ibada haramu ya sanamu;

Mwanzo 25 : 34
34 Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

Waraka kwa Waebrania 12 : 17
17 Maana mnajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.

Hesabu 11 : 4
4 Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, Ni nani atakayetupa nyama tule?

Zaburi 78 : 18
18 Wakamjaribu Mungu mioyoni mwao Kwa kutaka chakula kwa tamaa zao.

1 Samweli 2 : 17
17 ④ Hivyo dhambi yao wale vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa BWANA; kwa maana hao watu walidharau sadaka ya BWANA.

Danieli 5 : 1
1 ⑤ Mfalme Belshaza, aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa akanywa divai mbele ya hao elfu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *