Biblia inasema nini kuhusu ukoma – Mistari yote ya Biblia kuhusu ukoma

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ukoma

Mambo ya Walawi 14 : 1 – 57
1 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 ① Hii ndiyo sheria ya mwenye ukoma, katika siku ya kutakaswa kwake; ataletwa kwa kuhani,
3 na huyo kuhani atatoka aende nje ya kambi; na kuhani ataangalia, ikiwa pigo la ukoma limepoa kwake huyo mwenye ukoma;
4 ② ndipo huyo kuhani ataagiza kwamba watwae kwa ajili yake atakayetakaswa ndege wawili walio hai, ambao ni safi, na mti wa mwerezi, na sufu nyekundu, na hisopo;
5 kisha kuhani ataagiza ndege mmoja achinjwe katika chombo cha udongo kilicho juu ya maji ya mtoni;
6 kisha huyo ndege aliye hai atamshika, na huo mti wa mwerezi, na hiyo sufu nyekundu, na hisopo, naye atavichovya, pamoja na yule ndege aliye hai, katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa juu ya maji ya mtoni;
7 ③ kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba ni safi, kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani.
8 ④ Naye huyo atakayetakaswa atazifua nguo zake, na kunyoa nywele zake zote, na kuoga katika maji, naye atakuwa safi; baada ya hayo ataingia ndani ya kambi, lakini ataketi nje ya hema yake muda wa siku saba.
9 Kisha siku ya saba atanyoa nywele zote za kichwani mwake, na ndevu zake, na nyusi zake, nywele zake zote pia atazinyoa; kisha atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa safi.
10 ⑤ Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo wawili wa kiume wasio na dosari, na mwana-kondoo mmoja wa kike wa mwaka wa kwanza asiye na dosari, na sehemu tatu za kumi za efa[3] moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi[4] moja ya mafuta.
11 Kisha kuhani atakayemtakasa atamsimamisha huyo mtu atakayetakaswa, pamoja na vitu vile vyote, mbele za BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania;
12 ⑥ kisha kuhani atamshika mmoja kati ya hao wana-kondoo wa kiume, na kumsongeza awe sadaka ya hatia, pamoja na hiyo logi ya mafuta, kisha atavitikisa kuwa ni sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA;
13 ⑦ kisha atamchinja huyo mwana-kondoo mahali hapo wachinjiapo sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, ndani ya mahali patakatifu; kwa kuwa kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo ya kuhani, ndivyo ilivyo sadaka ya hatia; ni takatifu sana;
14 ⑧ kisha huyo kuhani atatwaa baadhi ya hiyo damu ya sadaka ya hatia, naye kuhani ataitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;
15 kisha kuhani atatwaa katika hiyo logi ya mafuta, na kuyamimina katika kitanga cha mkono wake mwenyewe wa kushoto;
16 kisha kuhani atatia kidole cha mkono wa kulia katika hayo mafuta, yaliyo katika mkono wake wa kushoto, naye atayanyunyiza hayo mafuta kwa kidole chake mara saba mbele za BWANA;
17 ⑩ na katika yale mafuta yaliyobaki mkononi mwake kuhani atayatia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia, juu ya damu ya sadaka ya hatia;
18 ⑪ na mafuta yaliyobaki, yaliyo katika mkono wa kuhani, atayatia juu ya kichwa cha huyo atakayetakaswa; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, mbele za BWANA.
19 Kisha kuhani atasongeza sadaka ya dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili yake huyo atakayetakaswa kwa sababu ya unajisi wake; kisha baadaye ataichinja sadaka ya kuteketezwa;
20 kisha kuhani ataisongeza hiyo sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, juu ya madhabahu na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.
21 ⑫ Lakini akiwa ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana-kondoo mmoja wa kiume, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta;
22 ⑬ na hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kama awezavyo kuwapata; huyo mmoja atakuwa sadaka ya dhambi, na wa pili atakuwa sadaka ya kuteketezwa.
23 Hata siku ya nane atawaleta kwa kuhani, mlangoni pa hema ya kukutania mbele za BWANA, kwa ajili ya kutakaswa kwake.
24 Na kuhani atamtwaa huyo mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na hiyo logi ya mafuta, naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA;
25 ⑭ kisha atamchinja mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na kuhani atatwaa katika damu ya sadaka ya hatia, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;
26 kisha kuhani atajimiminia baadhi ya mafuta hayo katika kitanga cha mkono wake wa kushoto;
27 kisha kuhani atanyunyiza baadhi ya hayo mafuta yaliyo katika mkono wake wa kushoto, kwa kidole chake cha mkono wa kulia mara saba mbele za BWANA;
28 ⑮ kisha kuhani atatia mengine katika hayo mafuta yaliyo mkononi mwake katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia, juu ya mahali pale penye damu ya sadaka ya hatia;
29 na mafuta yaliyobaki katika mkono wa kuhani atayatia juu ya kichwa cha huyo atakayetakaswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA.
30 ⑯ Kisha atasongeza hao hua mmojawapo, au hao makinda ya njiwa mmojawapo, kadiri ya awezao kuwapata;
31 hata kadiri aliyoweza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya unga; na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake huyo atakayetakaswa mbele za BWANA.
32 Huyo ambaye ndani yake mna pigo la ukoma, ambaye hawezi kukipata hicho kipasacho kutakaswa kwake, sheria yake ni hiyo.
33 BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
34 ⑰ Hapo mtakapoingia nchi ya Kanaani, ambayo nawapa kuwa ni milki yenu, nami nitakapolitia pigo la ukoma katika nyumba ya nchi hiyo ya milki yenu;
35 ⑱ ndipo mwenye nyumba hiyo atakwenda na kumwambia kuhani, akisema, Naona mimi ya kwamba pana kama pigo katika nyumba yangu;
36 ⑲ ndipo kuhani ataagiza kwamba watoe vyote vilivyomo nyumbani, kabla kuhani hajaingia ndani kuliangalia hilo pigo, ili vyote vilivyomo nyumbani visiwe najisi, kisha baadaye kuhani ataingia ndani ya nyumba hiyo aikague;
37 naye ataliangalia hilo pigo, na tazama, likiwa pigo limo ndani ya kuta za nyumba, nalo lina mashimo-mashimo, rangi ya majani, au mekundu, na kuonekana kuingia ndani kuliko huo ukuta;
38 ndipo kuhani atatoka katika nyumba hiyo mpaka mlangoni pa nyumba, na kuifunga hiyo nyumba muda wa siku saba;
39 siku ya saba kuhani atakwenda tena, naye ataangalia; na tazama, likiwa pigo limeenea katika kuta za nyumba;
40 ⑳ ndipo kuhani atawaambia wayatoe hayo mawe, yaliyo na pigo, na kuyatupa mahali penye uchafu nje ya mji;
41 naye atafanya kwamba hiyo nyumba ikwanguliwe ndani pande zote, na chokaa watakayokwangua wataimwaga nje ya mji mahali palipo na uchafu;
42 kisha watatwaa mawe mengine, na kuyatia mahali pa mawe hayo; naye atatwaa chokaa nyingine, na kuipaka chokaa hiyo nyumba.
43 Na kama hilo pigo likirudi tena, na kutokea ndani ya nyumba, baada ya yeye kuyatoa hayo mawe, na baada ya kuikwangua nyumba, na baada ya kupakwa chokaa,
44 ndipo kuhani ataingia ndani na kuangalia, likiwa pigo limeenea ndani ya hiyo nyumba, ni ukoma unaodhuru hiyo nyumba; ni unajisi.
45 Naye ataibomoa nyumba, mawe yake, na miti yake, na chokaa yote ya hiyo nyumba; naye atavichukua vyote nje ya mji hadi mahali palipo na uchafu.
46 Tena mtu atakayeingia ndani ya hiyo nyumba wakati huo wote iliofungwa, atakuwa najisi hadi jioni.
47 Na mtu alalaye ndani ya nyumba hiyo atazifua nguo zake, naye alaye chakula ndani ya nyumba hiyo atazifua nguo zake.
48 Kisha kuhani akiingia ndani kukagua na kuona kuwa pigo halikuenea katika hiyo nyumba baada ya nyumba kupakwa chokaa; ndipo kuhani atatangaza kuwa nyumba hiyo ni safi, maana pigo limepoa.
49 Naye atatwaa ndege wawili, na mti wa mwerezi, na sufu nyekundu, na hisopo, kwa kuitakasa hiyo nyumba;
50 naye atamchinja mmojawapo wa ndege hao katika chombo cha udongo kilicho juu ya maji ya mtoni;
51 kisha atatwaa huo mti wa mwerezi, na hisopo, na sufu nyekundu, pamoja na huyo ndege aliye hai, na kuvichovya vyote katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa, na katika hayo maji ya mtoni, na kuinyunyizia nyumba mara saba;
52 naye ataitakasa hiyo nyumba kwa damu ya ndege, na kwa maji ya mtoni, na kwa huyo ndege aliye hai, na kwa mti wa mwerezi, na kwa hisopo, na kwa sufu nyekundu;
53 lakini ndege aliye hai atamwacha atoke mle mjini aende nyikani; ndivyo atakavyofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo nyumba; nayo itakuwa safi.
54 Hiyo ndiyo sheria ya pigo la ukoma ya kila aina, na ya kipwepwe;
55 na ya ukoma wa vazi, na ukoma wa nyumba;
56 na kivimbe, na kikoko na kipaku king’aacho;
57 ili kufunza itakapokuwa ni unajisi, na itakapokuwa ni safi; hiyo ndiyo sheria ya ukoma.

Marko 1 : 40 – 42
40 Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa.
41 Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.
42 Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.

Mambo ya Walawi 13 : 46
46 Kwa siku zote ambazo pigo litakuwa ndani yake atakuwa najisi, ataishi kwa upweke katika makazi yake, nje ya kambi.

Luka 17 : 14
14 Alipowaona aliwaambia, Nendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.

Hesabu 5 : 1 – 3
1 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma[11] kambini, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya maiti;
3 mtawatoa nje wote, wanaume kwa wanawake, mtawaweka nje ya kambi; ili wasizitie unajisi kambi zao, ambazo mimi naketi katikati yazo.

Mambo ya Walawi 13 : 1 – 57
1 Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
2 Mtu atakapokuwa na uvimbe katika ngozi ya mwili wake, au upele, au kipaku king’aacho, nao ukawa ni ugonjwa wa ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa mmojawapo wa wanawe makuhani;
3 na huyo kuhani ataliangalia hilo pigo lililo katika ngozi ya mwili; na nywele zilizoko katika hilo pigo zimegeuka kuwa nyeupe, na hilo pigo kuonekana kwake limeingia ndani kuliko ile ngozi ya mwili wake, ni pigo la ukoma hilo; na ikiwa nywele zilizoko katika sehemu zilizougua zimegeuka rangi na kuwa nyeupe, na hilo pigo kuonekana limeingia ndani kuliko ile ngozi ya mwili, hilo ni pigo[1] la ukoma,
4 Lakini ikiwa kipaku king’aacho katika ngozi ya mwili wake ni cheupe, na kuonekana si shimo la kuingia ndani kuliko ngozi wala nywele hazikugeuka kuwa nyeupe, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba huyo aliye na hilo pigo;
5 kisha kuhani atamwangalia siku ya saba; naye akiona ya kuwa pigo limezuilika, na halikuenea katika ngozi yake, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba tena;
6 kisha siku ya saba kuhani atamwangalia tena; ikiwa hilo pigo limeanza kufifia, wala pigo halikuwa katika ngozi yake ndipo kuhani atasema kuwa ni mzima, ni kipele tu; naye atazifua nguo zake, kisha atakuwa ni safi.
7 Lakini ikiwa kipele kimeenea katika ngozi yake baada ya kujionesha kwa kuhani ili kutakaswa, atamwendea kuhani tena;
8 naye kuhani ataangalia, ikiwa huo upele umeenea katika ngozi, ndipo kuhani atasema kuwa ni najisi; ni ukoma.
9 Mtu atakapopatwa na ugonjwa wa ukoma, ndipo ataletwa kwa kuhani;
10 naye kuhani ataangalia, ikiwa pana uvimbe mweupe katika ngozi yake, na mnywele zimegeuzwa kuwa nyeupe, tena ikiwa panafanyika kidonda katika ule uvimbe,
11 ni ukoma usiopona ulio katika ngozi ya mwili wake, na kuhani atasema kuwa ni najisi; hatamweka mahali, kwa kuwa yeye ana unajisi.
12 Huo ukoma ukitokeza katika ngozi ya mgonjwa, na ukaenea katika ngozi yake yote, kutoka kichwani hadi miguuni, kama kuhani atakavyoweza kuona,
13 ndipo huyo kuhani ataangalia; ikiwa ukoma umemwenea mwili wake wote, atasema kuwa ni safi huyo aliye na hilo pigo, ikiwa ngozi yake yote imegeuka kuwa nyeupe, naye akawa safi.
14 Lakini popote kitakapoonekana kidonda kibichi kwake mtu huyo, atakuwa yu najisi.
15 Kuhani atakiangalia hicho kidonda kibichi, naye atasema kuwa ni najisi; kile kidonda kibichi ni najisi; ni ukoma.
16 Au kama hicho kidonda kibichi kinageuka tena na kuwa cheupe,[2] ndipo atamwendea kuhani,
17 na huyo kuhani atamwangalia; ikiwa hilo pigo limegeuzwa kuwa jeupe, ndipo huyo kuhani atasema kuwa huyo aliyekuwa na pigo ni safi.
18 Tena mwili wa mtu utakapokuwa na jipu katika ngozi yake, nalo limepoa,
19 na mahali palipokuwa na lile jipu pana uvimbe mweupe, au kipaku king’aacho, cheupe lakini chekundu kidogo, ndipo atamwonesha kuhani mahali hapo;
20 na kuhani ataangalia, kama kutaonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe, na malaika yakiwa yamegeuka kuwa meupe, ndipo kuhani atasema kwamba ni najisi; ni pigo la ukoma limetokea katika hilo jipu.
21 Lakini kuhani akipaangalia, na iwe hamna nywele nyeupe ndani yake, wala hapakuingia ndani kuliko ile ngozi, lakini paanza kufifia, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;
22 na kwamba pameenea katika ngozi, ndipo kuhani atasema kwamba ni najisi; hili ni pigo.
23 Lakini ikiwa kipaku hicho king’aacho kimekaa pale pale, wala hakienei, ni kovu ya jipu; na kuhani atasema kwamba yu safi.
24 Au mwili wa mtu ukiwa una mahali palipoungua katika ngozi yake, kisha pakawa kidonda, kikawa kipaku chekundu kidogo, au cheupe;
25 ndipo kuhani atapaangalia; ikiwa nywele iliyo katika kile kipaku imegeuka kuwa nyeupe, na kwamba kumeonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe; ni ukoma, umetokea katika mahali palipoungua; na kuhani atasema kuwa ni najisi; hili ni pigo la ukoma.
26 Lakini kuhani akipaangalia, nywele nyeupe hamna katika hicho kipaku king’aacho, nacho hakikuingia ndani kuliko ngozi, lakini chafifia; ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;
27 na kuhani atamwangalia siku ya saba; kama kimeenea katika ngozi, ndipo huyo kuhani atasema kuwa ni najisi; hili ni pigo la ukoma.
28 Na kama hicho kipaku kikibaki pale pale, wala hakikuenea katika ngozi, lakini kimefifia; ni kufura kwake pale penye moto, na kuhani atasema kuwa ni safi; kwa kuwa ni kovu la kuwasha hili.
29 Mwanamume au mwanamke atakapopatwa na maradhi kichani au kidevuni,
30 ndipo kuhani ataliangalia hilo pigo; ikiwa pigo limeingia ndani kuliko ngozi yenyewe, na nywele zilizomo kuwa za rangi ya manjano na nyembamba, ndipo kuhani atasema kwamba ni najisi, maana ni kipwepwe, ni ukoma wa kichwa au wa kindevu.
31 Tena kuhani akiliangalia lile pigo la kipwepwe, ikiwa kumeonekana si kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe, wala hamna nywele nyeusi ndani yake, ndipo kuhani atamweka mahali huyo aliye na pigo la kipwepwe muda wa siku saba;
32 na siku ya saba kuhani ataliangalia hilo pigo; na ikiwa hicho kipwepwe hakikuenea, wala hamna nywele za rangi ya manjano ndani yake, na kwamba kipwepwe hakionekani kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe,
33 ndipo huyo mtu atanyolewa, lakini hicho kipwepwe hatakinyoa; na kuhani atamweka mahali huyo aliye na kipwepwe muda wa siku saba tena;
34 na siku ya saba kuhani atakiangalia hicho kipwepwe, ikiwa kipwepwe hakikuenea katika ngozi yake, wala hakionekani kuingia ndani kuliko ngozi; ndipo huyo kuhani atasema kwamba ni safi; naye atazifua nguo zake, naye atakuwa ni safi.
35 Lakini hicho kipwepwe kama kikienea katika ngozi yake baada ya kutakasika kwake;
36 ndipo kuhani atamwangalia; na ikiwa hicho kipwepwe kimeenea katika ngozi yake, kuhani hatatafuta hizo nywele za rangi ya manjano; yeye ni najisi.
37 Lakini akiona ya kuwa hicho kipwepwe kimepungua, na nywele nyeusi zimemea humo; hicho kipwepwe kimepoa, naye yu safi, na huyo kuhani atasema kwamba yu safi.
38 Mwanamume au mwanamke, atakapokuwa na vipaku ving’aavyo katika ngozi ya mwili, vipaku ving’aavyo vyeupe;
39 ndipo kuhani ataangalia; ikiwa vile vipaku ving’aavyo vilivyo katika ngozi ya mwili wake ni vyeupe kidogo; ni mba iliyotokeza katika ngozi; yeye ni safi.
40 Kwamba nywele za mtu zimemtoka kichwani mwake, yeye ni mwenye upara, ni safi.
41 Tena kwamba nywele za mtu zimemtoka kichwani upande wa mbele, yeye ni mwenye upara wa kipaji; ni safi.
42 Lakini kwamba katika kile kichwa kilicho na upara, au kile kipaji kilicho na upara, laonekana pigo jeupe kisha jekundu kidogo; ni ukoma, unatokea katika kichwa chake cha upara, au katika kipaji chake cha upara.
43 Ndipo kuhani atamwangalia; kivimbe cha pigo kikiwa cheupe na chekundu chekundu, katika kichwa chake chenye upara, au katika kipaji chake cha upara, kama vile kuonekana kwa ukoma katika ngozi ya mwili;
44 yeye ni mtu mwenye ukoma, ni najisi; na kuhani hana budi atasema kuwa ni najisi; pigo lake liko katika kichwa chake.
45 Mtu mwenye ukoma aliye na pigo ndani yake, atavaa nguo zilizoraruka, na nywele timutimu; na ataufunika mdomo wake wa juu na kusema, “Ni najisi, ni najisi”.
46 Kwa siku zote ambazo pigo litakuwa ndani yake atakuwa najisi, ataishi kwa upweke katika makazi yake, nje ya kambi.
47 Kuhusu mavazi; vazi ambalo pigo la ukoma limo ndani yake, liwe ni vazi la sufu au la katani;
48 likiwa limefumwa, au kusokotwa; likiwa ni la kitani au la sufu; liwe katika ngozi, au kitu chochote kilichofanywa cha ngozi;
49 hilo pigo likiwa la rangi ya kijani au jekundu, katika vazi, au katika ngozi, au katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi; ni pigo la ukoma, nalo ataoneshwa kuhani;
50 na kuhani ataliangalia hilo pigo, naye atakiweka mahali kile kilicho na pigo muda wa siku saba;
51 kisha siku ya saba ataliangalia hilo pigo; kama pigo limeenea katika hilo lililofumwa, au katika hilo lililosokotwa, au katika ngozi, ijapokuwa hiyo ngozi ina matumizi yoyote; hilo pigo ni ukoma unaona; vazi hilo ni najisi.
52 Naye ataliteketeza vazi hilo, liwe ni la kufumwa au ni la kusokotwa, kama ni la sufu, au la kitani, au kitu chochote cha ngozi, ambacho kina hilo pigo ndani yake; kwa maana, ni ukoma unaona; vazi hilo litateketezwa;
53 Na kama kuhani akitazama, ikiwa hilo pigo halikuenea katika hilo vazi, wala katika hilo lililofumwa, wala katika hilo lililosokotwa, wala katika kitu chochote cha ngozi;
54 ndipo kuhani ataamuru kwamba wakifue kitu kile kilicho na hilo pigo, naye atakiweka mahali muda wa siku saba tena;
55 kisha kuhani ataangalia, baada ya kuoshwa hilo pigo; ikiwa hilo pigo halikugeuka rangi yake, wala halikuenea, ni najisi; utaliteketeza; ni uharibifu likiwa lina doa ndani au nje.
56 Huyo kuhani ataangalia, ikiwa hilo pigo limeanza kufifia, baada ya kufuliwa kwake, ndipo atalirarua hilo pigo litoke katika vazi, au katika ngozi, au katika lililofumwa, au katika lililosokotwa;
57 kisha, likionekana liko vile vile katika hilo vazi, katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi, ni pigo lenye kuenea; nawe vazi hilo lenye pigo utaliteketeza.

Mambo ya Walawi 13 : 45 – 46
45 Mtu mwenye ukoma aliye na pigo ndani yake, atavaa nguo zilizoraruka, na nywele timutimu; na ataufunika mdomo wake wa juu na kusema, “Ni najisi, ni najisi”.
46 Kwa siku zote ambazo pigo litakuwa ndani yake atakuwa najisi, ataishi kwa upweke katika makazi yake, nje ya kambi.

Luka 17 : 12 – 14
12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,
13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
14 Alipowaona aliwaambia, Nendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.

Mathayo 10 : 8
8 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

2 Wafalme 5 : 27
27 ⑮ Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.

Luka 5 : 14
14 ④ Akamkataza asimwambie mtu, ila, Nenda ukajioneshe kwa kuhani; ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao.

Hesabu 5 : 2
2 Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma[11] kambini, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya maiti;

Luka 5 : 13
13 Naye akaunyosha mkono wake, akamgusa akisema, Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukamwondoka.

Mathayo 8 : 3
3 Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika.

Mathayo 8 : 4
4 Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila nenda zako, ukajioneshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.

2 Mambo ya Nyakati 26 : 23
23 ⑬ Basi Uzia akalala na babaze; wakamzika karibu na babaze katika eneo la kuzikia la wafalme; kwa kuwa walisema, Huyu ni mwenye ukoma. Na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake.

2 Wafalme 7 : 3
3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?

Hesabu 12 : 1 – 10
1 Kisha Miriamu na Haruni wakamteta Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.
2 Wakasema, Je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao.
3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole[22] sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.
4 ① BWANA akanena ghafla na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.
5 ② BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.
6 ③ Kisha akawaambia, Sikilizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto.
7 ④ Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
8 ⑤ Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumteta mtumishi wangu, huyo Musa?
9 Hasira za BWANA zikawaka juu yao; kisha akaenda zake.
10 ⑥ Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na na kumwona akiwa mwenye ukoma.

2 Wafalme 5 : 1 – 27
1 Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
2 Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani.
3 Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake.
4 Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi.
5 ① Mfalme wa Shamu akasema, Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalme wa Israeli waraka. Basi akaenda zake, akachukua mikononi mwake talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu elfu sita, na mavazi kumi.
6 Akampelekea mfalme wa Israeli waraka ule, kusema, Waraka huu utakapokuwasilia, tazama, nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake.
7 ② Ikawa, mfalme wa Israeli alipousoma waraka, alirarua mavazi yake, akasema, Je! Mimi ni Mungu, niue na kuhuisha, hata mtu huyu akanipelekea mtu nimponye ukoma wake? Fahamuni, basi, nakusihini, mwone ya kuwa mtu huyu anataka kugombana nami.
8 ③ Ikawa, Elisha, yule mtu wa Mungu, aliposikia kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake, ndipo akatuma mtu kwa mfalme, akisema, Mbona umeyararua mavazi yako? Na aje sasa kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli.
9 Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha.
10 ④ Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Nenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi.
11 ⑤ Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nilidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la BWANA, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma.
12 ⑥ Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira.
13 Watumishi wake wakamkaribia, wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi?
14 ⑦ Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.
15 ⑧ Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani kote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee zawadi kutoka mtumwa wako.
16 ⑩ Lakini akasema, Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.
17 Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa BWANA.
18 ⑪ Jambo hili BWANA amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, BWANA amwachilie mtumwa wako jambo hili.
19 Elisha akamwambia, Nenda kwa amani. Lakini Naamani alipokuwa ameenda mbali kidogo,
20 ⑫ Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama BWANA aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake.
21 Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani?
22 Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.
23 Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamsihi, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakatangulia mbele yake wakiwa wameyabeba.
24 Naye alipofika kilimani, alivichukua kutoka mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao.
25 ⑬ Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali.
26 ⑭ Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi?
27 ⑮ Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.

2 Wafalme 15 : 1 – 360

1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli Uziaf[9] mwana wa Amazia mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
2 Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na miwili huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu.
3 Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, kama yote aliyoyafanya babaye Amazia.
4 Ila mahali pa juu hapakuondolewa, nao watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
5 BWANA akampiga mfalme, akawa na ukoma hata siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee. Na Yothamu mwana wa mfalme alikuwa juu ya nyumba, akiwahukumu watu wa nchi.
6 Basi mambo yote ya Uzia yaliyosalia, nayo yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?
7 Uzia akalala na babaze; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi; na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake.
8 Katika mwaka wa thelathini na nane wa Uzia mfalme wa Yuda Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria miezi sita.
9 Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA kama walivyofanya babaze; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.
10 Na Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya fitina juu yake, akampiga mbele ya watu, akamwua, akatawala mahali pake.
11 Basi mambo yote ya Zekaria yaliyosalia, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli.
12 Hilo ndilo neno la BWANA alilomwambia Yehu, akisema, Wana wako watakaa kitini mwa Israeli hata kizazi cha nne. Ikawa vivyo hivyo.
13 Huyo Shalumu mwana wa Yabeshi alianza kutawala katika mwaka wa thelathini na tisa wa Uzia mfalme wa Yuda; akatawala muda wa mwezi mmoja katika Samaria.
14 Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza, akaja Samaria, akampiga Shalumu mwana wa Yabeshi huko Samaria, akamwua, akatawala mahali pake.
15 Basi mambo yote ya Shalumu yaliyosalia, na njama alizozifanya, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli.
16 Ndipo Menahemu akapiga Tifsa, na wote waliokuwamo, na mipaka yake, toka Tirza; kwa sababu hawakumfungulia, kwa hiyo akaupiga; nao wanawake wote waliokuwamo wenye mimba akawapasua.
17 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa Uzia mfalme wa Yuda Menahemu mwana wa Gadi alianza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka kumi katika Samaria.
18 Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA; hakuyaacha siku zake zote makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.
19 Akaja Pulu mfalme wa Ashuru juu ya nchi; naye Menahemu akampa Pulu talanta elfu moja za fedha, ili kwamba mkono wake uwe pamoja naye, na ufalme uwe imara mkononi mwake.
20 Na Menahemu akawatoza Israeli fedha hiyo, yaani, matajiri wote wenye mali, kila mtu shekeli hamsini za fedha, ili ampe huyo mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akarejea, wala hakukaa huko katika nchi.
21 Basi mambo yote ya Menahemu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?
22 Menahemu akalala na babaze; na Pekahia mwanawe akatawala mahali pake.
23 Katika mwaka wa hamsini wa Uzia mfalme wa Yuda Pekahia mwana wa Menahemu alianza kutawala juu ya Israeli hatika Samaria; akatawala miaka miwili.
24 Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.
25 Na Peka mwana wa Remalia, jemadari wake, akamfanyia uhaini, akampiga huko Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme, pamoja na Argobu na Arie; na pamoja naye walikuwako watu hamsini wa Wagileadi. Akamwua, akatawala mahali pake.
26 Basi mambo yote ya Pekahia yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli.
27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Uzia mfalme wa Yuda Peka mwana wa Remalia alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka ishirini.
28 Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.
29 Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.
30 Na Hoshea mwana wa Ela akamfitinia Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
31 Basi mambo yote ya Peka yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, tazama, yameandikwa katika Iitabu cha Kumbukumbu cha Wafalme wa Israeli.
32 Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda alianza kutawala.
33 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Yerusha binti Sadoki.
34 Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA; akafanya kama yote aliyoyafanya Uzia baba yake.
35 Ila mahali pa juu hapakuondolewa; watu walikuwa wakitoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu. Ndiye aliyelijenga lango la juu la nyumba ya BWANA.
36 Basi mambo yote ya Yothamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?
37 Zamani hizo akaanza BWANA kumtuma juu ya Yuda Resini mfalme wa Shamu, na Peka mwana wa Remalia.
38 Yothamu akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi baba yake. Na Ahazi mwanawe akatawala mahali pake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *