Biblia inasema nini kuhusu ukimya – Mistari yote ya Biblia kuhusu ukimya

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ukimya

Maombolezo 3 : 26
26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu.

Zaburi 46 : 10
10 ⑰ Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.

Zaburi 62 : 5
5 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu. Maana tumaini langu hutoka kwake.

Ayubu 29 : 21
21 Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja, Wakanyamaza kimya wapate kusikia mashauri yangu.

Mithali 17 : 28
28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

Zaburi 141 : 3
3 Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

Mathayo 11 : 15
15 Mwenye masikio, na asikie.

Isaya 53 : 7
7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.

Warumi 10 : 17
17 Basi imani, hutokana na kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Ufunuo 8 : 1
1 Na Mwana-kondoo alipofungua mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa kama nusu saa.

Zaburi 62 : 1
1 Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa utulivu, Wokovu wangu hutoka kwake.

Mithali 18 : 13
13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.

Mithali 12 : 23
23 Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.

Wafilipi 4 : 11 – 12
11 Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yoyote niliyo nayo.
12 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yoyote, na katika mambo yoyote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.

Zaburi 141 : 3 – 4
3 Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.
4 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *