Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ukatili wa wanyama
Mithali 12 : 10
10 Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili.
Mhubiri 3 : 19
19 ⑲ Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.
Mithali 27 : 23
23 Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng’ombe wako.
Kutoka 23 : 5
5 Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye akiwa ameanguka chini ya mzigo wake, na wewe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
Mwanzo 1 : 28
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Zaburi 145 : 9
9 ⑪ BWANA ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake ziko juu ya vyote alivyoumba.[25]
Isaya 1 : 11
11 Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema BWANA. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo dume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng’ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi dume.
Mwanzo 1 : 30
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
Luka 12 : 6
6 Je! Shomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu.
Kumbukumbu la Torati 25 : 4
4 ⑲ Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa.
Luka 15 : 4 – 7
4 ⑬ Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na tisa nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hadi amwone? ⑭
5 Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi.
6 Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.
7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.
Leave a Reply