Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ukamilifu
Mwanzo 6 : 9
9 ① Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.
Hesabu 23 : 21
21 ⑧ Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. BWANA, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme iko katikati yao.
1 Wafalme 11 : 4
4 ③ Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.
1 Wafalme 11 : 6
6 ⑤ Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
1 Wafalme 15 : 14
14 ⑬ Lakini mahali pa juu hapakuondoshwa; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu kwa BWANA siku zake zote.
Ayubu 1 : 1
1 Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
Luka 1 : 6
6 Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiishi katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.
Yohana 1 : 47
47 ⑫ Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.
Mwanzo 17 : 1
1 ⑥ Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Kumbukumbu la Torati 5 : 32
32 ⑲ Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kulia wala wa kushoto.
Kumbukumbu la Torati 18 : 13
13 ⑮ Uwe mkamilifu kwa BWANA, Mungu wako.
Yoshua 23 : 6
6 Basi, iweni thabiti sana kuyashika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, na kuyatenda, msiyaache kwa kugeukia upande wa kulia wala upande wa kushoto.
1 Wafalme 8 : 61
61 ⑫ Mioyo yenu na iwe kamili kwa BWANA, Mungu wetu, kuenenda katika sheria zake, na kuzishika amri zake, kama ilivyo leo.
1 Mambo ya Nyakati 28 : 9
9 ⑦ Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
1 Mambo ya Nyakati 29 : 19
19 naye Sulemani mwanangu, umjalie ili kwa moyo wote, azishike amri zako, na shuhuda zako, na maagizo yako, akayatende hayo yote na kuijenga nyumba hii ya enzi, niliyoiwekea akiba.
2 Mambo ya Nyakati 6 : 36
36 ⑭ Wakikukosa, (maana hakuna mtu asiyekosa), hata uwakasirikie, na kuwatia mikononi mwa adui zao, wawahamishe, na kuwachukua mateka mpaka nchi iliyo mbali au iliyo karibu;
Ayubu 9 : 21
21 Mimi ni mkamilifu; siangalii nafsi yangu; Naudharau uhai wangu.
Zaburi 18 : 32
32 Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu.
Zaburi 37 : 31
31 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake. Hatua zake hazitelezi.
Zaburi 37 : 37
37 Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
Zaburi 101 : 2
2 Nitakuwa na mwenendo usio na hatia; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu.
Zaburi 106 : 3
3 Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote.
Zaburi 119 : 3
3 Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake.
Leave a Reply