Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ujinga
Ayubu 8 : 9
9 (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)
Ayubu 11 : 8
8 Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?
Ayubu 11 : 12
12 Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu, Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda mwitu.
Ayubu 28 : 13
13 Mwanadamu hajui thamani yake, Wala haionekani katika nchi ya walio hai.
Ayubu 28 : 21
21 Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani.
Ayubu 36 : 26
26 Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; Hesabu ya miaka yake haichunguziki.
Ayubu 36 : 29
29 Naam, mtu aweza kuelewa matandazo ya mawingu, Ngurumo za makao yake?
Ayubu 37 : 5
5 Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuyaelewa.
Ayubu 37 : 16
16 Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?
Ayubu 37 : 19
19 Utufundishe ni maneno gani tutakayomwambia; Kwa kuwa hatuwezi kutoa hoja zetu maana tumo gizani.
Ayubu 37 : 23
23 Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.
Zaburi 139 : 6
6 Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.
Mithali 7 : 23
23 Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
Mithali 8 : 5
5 Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu.
Mithali 9 : 18
18 Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni.
Mithali 19 : 2
2 Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi.
Mithali 20 : 24
24 ⑭ Mwenendo wa mtu watoka kwa BWANA; Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake?
Mithali 22 : 3
3 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
Mithali 27 : 12
12 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
Mithali 27 : 1
1 Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.
Mithali 30 : 4
4 ⑱ Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
Mhubiri 3 : 11
11 ⑬ Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
Mhubiri 6 : 12
12 Kwa maana ni nani ajuaye yaliyo mema ya mwanadamu katika maisha yake, siku zote za maisha yake ya ubatili, anayoishi kama kivuli? Kwa maana ni nani awezaye kumweleza mwanadamu mambo yatakayofuata baada yake chini ya jua?
Mhubiri 7 : 24
24 ⑧ Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana, ni mtu yupi awezaye kuyatafuta?
Mhubiri 8 : 7
7 ⑭ kwa kuwa hajui yatakayokuwako; kwa maana ni nani awezaye kumweleza jinsi yatakavyokuwa?
Mhubiri 8 : 17
17 basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haifahamiki na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu hata mwanadamu akijisumbua kadiri awezavyo kuichunguza, hataiona; naam, zaidi ya hayo, hata ingawa mwenye hekima hadai anajua, wao hawawezi kuifahamu.
Mhubiri 9 : 12
12 Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafla.
Leave a Reply