Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ujanja
Kutoka 21 : 11
11 Ikiwa hamfanyii mambo haya matatu, ndipo atatoka aende bure, pasipo kutolewa mali.
Mambo ya Walawi 19 : 22
22 Kisha huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia mbele za BWANA, kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya; naye atasamehewa hiyo dhambi yake aliyoifanya.
Kumbukumbu la Torati 21 : 14
14 ⑦ Tena utakapokuwa huna furaha naye, mpe ruhusa aende atakako; lakini usimwuze kabisa kwa fedha, usimfanye kama mtumwa, kwa kuwa ulimtweza.
Mwanzo 21 : 14
14 ⑩ Abrahamu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akamtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
Mwanzo 37 : 2
2 Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya.
Waamuzi 19 : 5
5 ③ Kisha ilikuwa siku ya nne, wakaamka asubuhi na mapema, naye akaondoka ili aende zake; baba yake huyo mwanamke akamwambia mkwewe, Tunza moyo wako, ule chakula kidogo, kisha baadaye mtakwenda zenu.
Mwanzo 15 : 4
4 Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali utakayemzaa ndiye atakayekurithi.
Mwanzo 21 : 10
10 ⑤ Kwa hiyo akamwambia Abrahamu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.
Mwanzo 16 : 3
3 Kwa hiyo, baada ya Abramu kukaa miaka kumi katika nchi ya Kanaani, Sarai mkewe Abramu alimtwaa Hajiri Mmisri, mjakazi wake, akampa Abramu mumewe, kama mke.
Mwanzo 25 : 6
6 ⑬ Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Abrahamu, Abrahamu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 32
32 Na wana wa Ketura, suria yake Abrahamu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.
Mwanzo 22 : 24
24 Na suria wake Reuma naye alizaa Teba na Gahamu na Tahashi na Maaka.
Mwanzo 30 : 4
4 Basi akampa Bilha mjakazi wake kuwa mkewe. Yakobo akaingia kwake.
Mwanzo 36 : 12
12 Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau.
Waamuzi 8 : 31
31 Na suria yake aliyekuwako Shekemu, yeye naye akamzalia mwana, naye akamwita jina lake Abimeleki.
Waamuzi 19 : 1
1 ② Ikawa katika siku hizo, kulipokuwa hakuna mfalme katika Israeli, alikuwapo Mlawi mmoja aliyekuwa akikaa kama mgeni upande wa mbele wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu, aliyejitwalia suria katika Bethlehemu-yuda.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 48
48 Naye Maaka, suria yake Kalebu, akamzalia Sheberi, na Tirhana.
1 Mambo ya Nyakati 7 : 14
14 Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi;
2 Samweli 3 : 7
7 ⑮ Basi Sauli alikuwa na suria, jina lake akiitwa Rispa, binti Aya; Ishboshethi akamwuliza Abneri, Kwa nini umeingia kwa suria ya babangu?
Leave a Reply