Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ujambazi
Mambo ya Walawi 19 : 13
13 ⑰ Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang’anya mali yake; ujira wake aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi.
Isaya 61 : 8
8 Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wizi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.
Ezekieli 18 : 10
10 ① Walakini akizaa mwana aliye mnyang’anyi, mmwaga damu, atendaye mambo hayo mojawapo;
Ezekieli 18 : 13
13 ④ naye amekopesha watu ili apate faida, na kupokea ziada; je! Ataishi baada ya hayo? La, hataishi; amefanya machukizo hayo yote; hakika atakufa; damu yake itakuwa juu yake.
Ezekieli 33 : 15
15 ⑲ kama mtu mwovu akirudisha rehani, na kumrudishia mtu mali yake aliyomnyang’anya, akizifuata sheria za uzima, asitende uovu wowote; hakika ataishi, hatakufa.
Waamuzi 9 : 25
25 Basi watu wa Shekemu wakaweka watu kumvizia juu ya vilele vya milima, ambao waliwapora watu wote waliopita njia hiyo karibu nao; naye Abimeleki aliarifiwa.
Leave a Reply