Biblia inasema nini kuhusu Uhaini – Mistari yote ya Biblia kuhusu Uhaini

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uhaini

Hesabu 12 : 11
11 ⑦ Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu,[23] kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.

Hesabu 16 : 33
33 Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wakiwa hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.

Waamuzi 1 : 25
25 Basi akawaonesha njia ya kuingia mji, nao wakaupiga huo mji kwa makali ya upanga; lakini huyo mtu walimwacha aende zake, na watu wote wa jamaa yake.

Waamuzi 9 : 25
25 Basi watu wa Shekemu wakaweka watu kumvizia juu ya vilele vya milima, ambao waliwapora watu wote waliopita njia hiyo karibu nao; naye Abimeleki aliarifiwa.

Waamuzi 12 : 4
4 ⑮ Ndipo Yeftha akawakutanisha watu wote wa Gileadi, na kupigana na Efraimu; na hao watu wa Gileadi wakawapiga Efraimu, kwa sababu walisema, Ninyi Wagileadi ni watoro mliotoroka Efraimu, na kukaa kati ya Efraimu na Manase.

1 Samweli 10 : 27
27 Lakini wengine wasiofaa kitu wakasema, Huyu je! Atatuokoaje? Nao wakamdharau, wasimletee zawadi.

1 Wafalme 12 : 19
19 Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi hata leo.

1 Samweli 30 : 16
16 Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.

2 Samweli 3 : 21
21 Kisha Abneri akamwambia Daudi, Nitaondoka, niende zangu; nami nitamkusanyia bwana wangu mfalme Israeli wote, ili wafanye agano nawe, ukamiliki juu ya wote inaowatamani roho yako. Basi Daudi akamruhusu Abneri; naye akaenda zake kwa amani.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *