Biblia inasema nini kuhusu Ugomvi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ugomvi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ugomvi

Mwanzo 13 : 8
8 ⑥ Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu jamaa moja.

Mwanzo 45 : 24
24 Akaagana na ndugu zake, wakaenda zao; naye akawaambia, Msigombane njiani.

Kumbukumbu la Torati 1 : 12
12 Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na ugomvi wenu?

Zaburi 31 : 20
20 Utawasitiri kutoka kwa fitina za watu Katika maficho ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na ushindani wa ndimi.

Zaburi 55 : 9
9 Ee Bwana, uwaangamize, uzivuruge ndimi zao, Maana nimeona dhuluma na fitina katika mji.

Zaburi 80 : 6
6 Unatufanya sababu ya ugomvi kwa jirani zetu, Na adui zetu wanacheka wao kwa wao.

Mithali 3 : 30
30 Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lolote.

Mithali 6 : 14
14 ③ Mna upotovu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi.

Mithali 6 : 19
19 ⑦ Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Mithali 10 : 12
12 ⑮ Kuchukiana huleta fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote.

Mithali 13 : 10
10 Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.

Mithali 15 : 18
18 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.

Mithali 16 : 28
28 Mtu mshupavu huleta fitina; Na mchongezi huwafarakanisha rafiki.

Mithali 17 : 1
1 Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.

Mithali 17 : 14
14 Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.

Mithali 17 : 19
19 Apendaye ugomvi hupenda dhambi; Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu.

Mithali 18 : 6
6 Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina, Na kinywa chake huita mapigo.

Mithali 18 : 19
19 Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.

Mithali 19 : 13
13 Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye; Na ugomvi wa mke kama kudondoka kwa matone daima.

Mithali 20 : 3
3 ④ Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana.

Mithali 21 : 19
19 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.

Mithali 22 : 10
10 Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma.

Mithali 23 : 30
30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.

Mithali 25 : 8
8 ⑬ Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha.

Mithali 25 : 24
24 Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.

Mithali 26 : 17
17 Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake.

Mithali 26 : 21
21 Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, Na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *