Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ufunuo
Kutoka 3 : 6
6 ⑩ Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akafunika uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.
Kutoka 3 : 14
14 ⑱ Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;[3] akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO[4] amenituma kwenu.
Kutoka 6 : 3
3 ⑮ nami nilimtokea Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi,[7] bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
1 Mambo ya Nyakati 28 : 19
19 ⑭ Hayo yote, akasema Daudi, yamenielea kwa maandiko kutoka kwa mkono wa BWANA, naam, kazi zote za mfano huu.
Mathayo 3 : 17
17 ⑭ na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Mathayo 16 : 17
17 ⑮ Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Baryona;[2] kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
Leave a Reply