Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Udhu
Kutoka 19 : 10
10 ② BWANA akamwambia Musa, Nenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao,
Kutoka 19 : 14
14 Musa akateremka mlimani akawaendea watu akawatakasa, nao wakafua nguo zao.
Mathayo 15 : 2
2 Mbona wanafunzi wako huyavunja mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.
Marko 7 : 5
5 Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi?
Marko 7 : 9
9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.
Luka 11 : 38
38 Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula.
Waraka kwa Waebrania 9 : 10
10 kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kunawa kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.
Kutoka 29 : 4
4 Kisha mlete Haruni na wanawe hata mlangoni pa hema ya kukutania, ukawaoshe kwa maji.
Kutoka 30 : 21
21 basi wataosha mikono yao na miguu yao ili kwamba wasife; na neno hili litakuwa amri kwao milele, kwake yeye na kwa wazao wake katika vizazi vyao vyote.
Kutoka 40 : 12
12 Kisha utamleta Haruni na wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji.
Kutoka 40 : 32
32 ③ hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa.
Mambo ya Walawi 8 : 6
6 Basi Musa akawaleta Haruni na wanawe, akawaosha kwa maji.
Mambo ya Walawi 16 : 4
4 ② Ataivaa ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake, atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani; hayo ndiyo mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini, na kuyavaa.
Mambo ya Walawi 16 : 24
24 naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na kuvaa nguo zake, na kutoka, na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe, na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu.
Mambo ya Walawi 16 : 26
26 Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika kambi.
Mambo ya Walawi 16 : 28
28 Na yeye awachomaye moto atafua nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia kambini.
Hesabu 19 : 10
10 Na yeye ayazoaye majivu ya huyo ng’ombe atazifua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; na jambo hili litakuwa amri ya milele, kwa wana wa Israeli, na wa mgeni akaaye kati yao.
Hesabu 19 : 19
19 ⑬ na yule aliye safi atamnyunyizia huyo aliye najisi siku ya tatu, na siku ya saba; na katika siku ya saba atamtakasa; naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa safi jioni.
2 Mambo ya Nyakati 4 : 6
6 ⑮ Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea.
Mambo ya Walawi 1 : 9
9 lakini matumbo yake, na miguu yake, ataiosha kwa maji; na huyo kuhani ataviteketeza vyote juu ya madhabahu, ili iwe sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.
Mambo ya Walawi 1 : 13
13 lakini matumbo yake, na miguu yake, ataosha kwa maji; na huyo kuhani atavisongeza vyote na kuviteketeza juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.
Mambo ya Walawi 9 : 14
14 Kisha akaosha matumbo, na miguu na kuiteketeza juu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa madhabahuni.
2 Mambo ya Nyakati 4 : 6
6 ⑮ Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea.
Matendo 9 : 37
37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; wakati walipokwisha kumwosha, wakamweka ghorofani.
Ezekieli 16 : 4
4 Na kuhusu habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.
Leave a Reply