Biblia inasema nini kuhusu ucheshi na kicheko – Mistari yote ya Biblia kuhusu ucheshi na kicheko

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ucheshi na kicheko

Mithali 17 : 22
22 Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.

Zaburi 126 : 2
2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, BWANA amewatendea mambo makuu.

Ayubu 8 : 21
21 Bado atakijaza kinywa chako kicheko, Na midomo yako ataijaza shangwe.

Mhubiri 3 : 4
4 ⑦ Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

Mithali 15 : 13
13 Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.

Zaburi 2 : 4
4 Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.

Mwanzo 21 : 6
6 ② Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami.

Zaburi 32 : 11
11 Mfurahieni BWANA; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.

Waefeso 5 : 4
4 wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali kuwepo kushukuru.

Zaburi 37 : 13
13 BWANA atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.

Mithali 14 : 13
13 Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.

Zaburi 16 : 11
11 ① Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.

Zaburi 16 : 8 – 11
8 Nimemweka BWANA mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa.
9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
10 Maana hutaitupa kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
11 ① Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.

Zaburi 4 : 7
7 Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.

Sefania 3 : 17
17 BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.

Wafilipi 4 : 4
4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.

Mwanzo 17 : 17
17 ⑲ Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?

Wakolosai 4 : 6
6 ⑥ Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Zaburi 47 : 1
1 Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.

Mithali 31 : 25
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *