Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ubinafsi
Wafilipi 2 : 4
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
1 Yohana 3 : 17
17 โณ Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?
1 Wakorintho 10 : 24
24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.
2 Timotheo 3 : 2 โ 4
2 โฉ Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
4 โช wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
Wafilipi 2 : 3 โ 4
3 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
Wafilipi 2 : 21
21 โฆ Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu.
Wagalatia 6 : 2
2 Mchukuliane mizigo na hivyo kuitimiza sheria ya Kristo.
Yakobo 4 : 1 โ 2
1 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?
2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
1 Wakorintho 13 : 4 โ 6
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
Warumi 15 : 1 โ 3
1 Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.
2 Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe.
3 Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Matusi yao waliokutusi wewe yalinipata mimi.
1 Timotheo 6 : 17 โ 19
17 โ Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.
18 Waamuru watende mema, wawe matajiri katika kutenda mema, wawe wakarimu na wawe tayari kushiriki na wengine;
19 โก huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Wagalatia 5 : 26
26 โฒ Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.
Mithali 28 : 27
27 Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.
Matendo 20 : 35
35 Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Hagai 1 : 9
9 Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha mbali. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu yumba yangu imebaki kuwa gofu la nyumba, wakati ambapo kila mmoja wenu anakimbilia nyumbani kwake.
Luka 6 : 32 โ 34
32 Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
33 Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.
Wagalatia 5 : 24
24 โฐ Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Mithali 21 : 13
13 โณ Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.
Yakobo 1 : 13 โ 15
13 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
Leave a Reply