Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ubaguzi
Wagalatia 3 : 28
28 Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.
Nehemia 13 : 23 – 30
23 Tena siku zizo hizo nikawaona wale Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake wa Ashdodi, na Amoni, na Moabu;
24 na nusu ya watoto wao wakazungumza kwa lugha ya Ashdodi, wala hawakuweza kuzungumza Kiyahudi, bali kwa lugha mojawapo ya watu hao.
25 Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang’oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.
26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; lakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.
27 Basi, na sisi, je! Tuwasikilize ninyi kutenda neno hili baya, hata kumkosea Mungu wetu kwa kuwaoa wanawake wageni?
28 Na mwana mmoja wa Yoyada, mwana wa Eliashibu, kuhani mkuu, alikuwa mkwewe Sanbalati, Mhoroni, basi nikamfukuza kwangu.
29 Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, jinsi walivyounajisi ukuhani, na agano la ukuhani na la Walawi.
30 ① Hivyo nikawatakasa na kila kitu kigeni, nami nikawawekea zamu makuhani na Walawi, kila mtu kazini mwake;
Kumbukumbu la Torati 23 : 2
2 Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa BWANA; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa BWANA.
Yeremia 2 : 21
21 Nami nilikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibumwitu machoni pangu?
Kumbukumbu la Torati 7 : 3
3 binti yako usimwoze kwao wala mtoto wako wa kiume kuoa kwao.
Leave a Reply