Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uasi
Wagalatia 1 : 8 – 9
8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria, na alaaniwe.
9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
Kumbukumbu la Torati 13 : 6 – 11
6 Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mama yako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;
7 katika miungu ya mataifa yaliyo kandokando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia;
8 usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;
9 mwue kweli; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote.
10 Nawe mtupie mawe hata afe; kwa kuwa alitaka kukupotoa na BWANA, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
11 Na Israeli wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako.
2 Mambo ya Nyakati 15 : 13
13 na ya kwamba yeyote asiyemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, awe ni mwanamume au mwanamke.
2 Petro 2 : 20 – 22
20 ⑤ Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
21 ⑥ Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
22 ⑦ Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni.
1 Timotheo 4 : 1
1 ⑫ Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
Waraka kwa Waebrania 6 : 4 – 8
4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za wakati ujao,
6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumtweza hadharani kwa dhahiri.
7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao inalimwa, hupokea baraka zitokazo kwa Mungu;
8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.
2 Petro 3 : 17
17 Basi, wapenzi kwa kuwa mmejua hayo, jihadharini msije mkapotoshwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthabiti wenu.
Mathayo 24 : 10
10 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.
2 Wathesalonike 2 : 3
3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
Luka 8 : 13
13 Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.
Waraka kwa Waebrania 10 : 26 – 29
26 ⑬ Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
27 ⑭ bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
28 ⑮ Mtu aliyeidharau Sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 ⑯ Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?
2 Timotheo 4 : 3
3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajikusanyia waalimu wengi, watakaowaambia yale tu masikio yao yanataka kusikia;
2 Timotheo 3 : 1 – 9
1 ⑧ Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 ⑩ Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
4 ⑪ wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
5 ⑫ walio na utaua kwa nje, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
6 ⑬ Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za kila namna;
7 ⑭ wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
8 ⑮ Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
9 Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao wanaume wawili[1] ulivyokuwa dhahiri.
Waraka kwa Waebrania 3 : 12
12 Hadharini, ndugu zangu, usiwepo katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutoamini, ujitengao na Mungu aliye hai.
Mathayo 24 : 12
12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapunguka.
Yohana 6 : 66
66 Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.
1 Timotheo 4 : 1 – 3
1 ⑫ Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 ⑬ wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
2 Timotheo 4 : 4
4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
2 Petro 2 : 1
1 Lakini kulitokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
Waraka kwa Waebrania 10 : 1 – 360
1 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wowote kuwakamilisha wakaribiao.
2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?
3 Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.
4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.
5 Kwa hiyo alipokuja ulimwenguni, alisema, Dhabihu na matoleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari;
6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;
7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la kitabu nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu.
8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati),
9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.
10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.
11 ① Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.
12 ② Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kulia wa Mungu;
13 tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake.
14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
15 Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema,
16 ③ Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika fikira zao nitaziandika; ndipo anenapo,
17 ④ Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
18 Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.
19 ⑤ Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,
20 ⑥ njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;
21 ⑦ na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;
22 ⑧ na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.
23 ⑩ Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu;
24 ⑪ tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;
25 ⑫ wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.
26 ⑬ Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
27 ⑭ bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
28 ⑮ Mtu aliyeidharau Sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 ⑯ Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?
30 ⑰ Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.
31 ⑱ Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.
32 ⑲ Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu;
33 ⑳ pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na dhiki, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo.
34 Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.
35 Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.
36 Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.
37 Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.
38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye.
39 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.
Leave a Reply