Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uadilifu
1 Yohana 4 : 7 – 10
7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
9 Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
Mithali 10 : 9
9 ⑬ Aendaye kwa unyofu huenda salama; Bali apotoshaye njia zake atajulikana.
Mithali 28 : 6
6 Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotovu wa njia angawa ni tajiri.
Mithali 11 : 3
3 Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.
Mithali 19 : 1
1 Afadhali maskini aendaye katika uadilifu wake, Kuliko mpotovu wa midomo aliye mpumbavu.
Mithali 12 : 22
22 ⑤ Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.
Mithali 20 : 7
7 Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, Watoto wake wabarikiwa baada yake.
1 Petro 3 : 16
16 Nanyi muwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.
Wakolosai 3 : 23
23 Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
Luka 16 : 10
10 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na asiyeaminika katika lililo dogo, huwa haaminiki pia katika lililo kubwa.
Mithali 21 : 3
3 ⑯ Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.
2 Wakorintho 8 : 21
21 tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
Tito 2 : 1 – 14
1 Lakini wewe, nena mambo yanayoambatana na mafundisho mema;
2 ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika subira.
3 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wanaofundisha yaliyo mema;
4 ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;
5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
6 Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi;
7 katika mambo yote ukijionesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionesha usahihi na ustahivu,
8 na maneno yafaayo yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.
9 Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wakaidi,
10 wasiwe wezi; bali wauoneshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mungu aliye Mwokozi wetu katika mambo yote.
11 Maana neema ya Mungu iwaokoao wanadamu wote imefunuliwa;
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na kufunuliwa kwa utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
14 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.
Waraka kwa Waebrania 13 : 18
18 ⑧ Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote.
Zaburi 41 : 11 – 12
11 Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami, Kwa kuwa adui yangu hajivunii kunishinda.
12 Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza, Umeniweka mbele za uso wako milele.
Wafilipi 4 : 8
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Mithali 4 : 25 – 27
25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
26 Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike;
27 Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni.
Luka 6 : 31
31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.
Ayubu 27 : 4 – 6
4 Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki, Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5 Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki; Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu.
6 Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha; Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.
Leave a Reply