Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia tohara
1 Wakorintho 7 : 19
19 Kutahiriwa si kitu, na kutotahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.
Mwanzo 21 : 4
4 ① Abrahamu akamtahiri Isaka mwanawe, alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwamuru.
Warumi 4 : 11
11 Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, mhuri wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;
Wagalatia 5 : 2 – 11
2 ① Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidi neno.
3 Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote.
4 Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.
5 Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.
6 ② Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
7 Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli?
8 ③ Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi.
9 ④ Chachu kidogo huchachua donge zima.
10 ⑤ Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewasumbua atachukua hukumu yake, awaye yote.
11 ⑥ Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Kwa kufanya hivyo kikwazo cha msalaba kimeondolewa!
Wagalatia 2 : 3
3 Lakini Tito aliyekuwa pamoja nami, naye ni Mgiriki, hakulazimishwa kutahiriwa.
Mwanzo 17 : 12
12 ⑯ Katika vizazi vyako vyote, kila mtoto wa kiume miongoni mwenu atatahiriwa akiwa na umri wa siku nane, awe mtumishi aliyezaliwa katika nyumba yako au uliyemnunua kwa fedha zako japo hakuwa wa uzao wako.
Waefeso 2 : 11
11 ⑥ Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;
Warumi 2 : 25 – 29
25 ⑮ Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutotahiriwa.
26 ⑯ Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! Kutotahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa?
27 Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaivunja torati?
28 ⑰ Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;
29 ⑱ bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Warumi 2 : 28
28 ⑰ Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;
Wafilipi 3 : 3
3 ⑭ Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.
Mwanzo 17 : 14
14 ⑰ Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.
Yeremia 4 : 4
4 Jitahirini kwa BWANA, mkayaondoe magovi ya mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
1 Wakorintho 7 : 18
18 Je! Mtu fulani ameitwa akiwa amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa akiwa hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe.
Wakolosai 2 : 11
11 ⑬ Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.
Matendo 15 : 1 – 41
1 ⑮ Wakashuka watu waliotoka Yudea wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamuwezi kuokoka.
2 ⑯ Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee ili kuzungumza juu ya suala hilo.
3 Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.
4 ⑰ Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.
5 Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.
6 Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulitafakari neno hilo.
7 ⑱ Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.
8 ⑲ Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi;
9 ⑳ wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.
10 Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulibeba.
11 Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.
12 Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa.
13 Na hao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akisema, Ndugu zangu, nisikilizeni.
14 Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.
15 Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa,
16 Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha;
17 Ili wanadamu waliobakia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao;
18 Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.
19 Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa;
20 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.
21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.
22 Basi ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao,
23 Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.
24 Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, ambao sisi hatukuwaagiza;
25 sisi tumeona vema, hali tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwatuma kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo,
26 watu waliohatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
27 Basi tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambia wenyewe maneno yayo hayo kwa vinywa vyao.
28 Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima,
29 yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
30 Hata hao wakiisha kupewa ruhusa wakateremka kwenda Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ile barua.
31 Nao walipokwisha kuisoma wakafurahi kwa ajili ya faraja ile.
32 Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha.
33 Na wakiisha kukaa huko muda, wakaruhusiwa na ndugu waende kwa amani kwa hao waliowatuma. [
34 Lakini Sila akaona vema kukaa huko.]
35 Na Paulo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisha na kulihubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.
36 Baada ya siku kadhaa Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Turejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wako hali gani.
37 Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao.
38 Bali Paulo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfilia, asiende nao kazini.
39 Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko akaabiri kwenda Kipro.
40 Lakini Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana.
41 Akapita katika Shamu na Kilikia akiyaimarisha makanisa.
Mwanzo 17 : 13
13 Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.
Wagalatia 6 : 15
15 Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutotahiriwa, ila kiumbe kipya.
Mwanzo 17 : 10 – 14
10 ⑭ Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati yangu nawe, na uzao wako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.
11 ⑮ Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.
12 ⑯ Katika vizazi vyako vyote, kila mtoto wa kiume miongoni mwenu atatahiriwa akiwa na umri wa siku nane, awe mtumishi aliyezaliwa katika nyumba yako au uliyemnunua kwa fedha zako japo hakuwa wa uzao wako.
13 Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.
14 ⑰ Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.
Wakolosai 2 : 11 – 12
11 ⑬ Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.
12 ⑭ Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.
Wagalatia 6 : 12
12 Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu.
Leave a Reply