Biblia inasema nini kuhusu Toba – Mistari yote ya Biblia kuhusu Toba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Toba

Mwanzo 6 : 7
7 BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewaumba.

Kutoka 32 : 14
14 Na BWANA akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.

Kumbukumbu la Torati 32 : 36
36 ② Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa,

Waamuzi 2 : 18
18 ⑭ Na kila wakati BWANA alipowainulia waamuzi, ndipo BWANA alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana BWANA alisikitishwa na kilio chao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.

1 Samweli 15 : 11
11 ⑮ Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha.

1 Samweli 15 : 29
29 Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute.

1 Samweli 15 : 35
35 Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye BWANA akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.

2 Samweli 24 : 16
16 ③ Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, BWANA akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa BWANA alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna,[20] Myebusi.

1 Mambo ya Nyakati 21 : 15
15 Naye Mungu akatuma malaika aende Yerusalemu ili auangamize; naye alipokuwa tayari kuangamiza, BWANA akatazama, akaghairi katika mabaya, akamwambia malaika aharibuye, Basi yatosha; sasa ulegeze mkono wako. Naye malaika wa BWANA akasimama karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna,[19] Myebusi.

Zaburi 106 : 45
45 ③ Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;

Zaburi 110 : 4
4 ⑦ BWANA ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.

Zaburi 135 : 14
14 Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake, Na kuwahurumia watumishi wake.

Yeremia 15 : 6
6 ⑧ Umenikataa mimi, asema BWANA, umerudi nyuma; ndiyo maana nimenyosha mkono wangu juu yako, na kukuangamiza; nimechoka kwa kughairi.

Yeremia 18 : 8
8 ⑫ ikiwa taifa lile nililolitaja litageuka, na kuacha maovu yake nitaghairi, nisitende mabaya yale niliyoazimia kuwatenda.

Yeremia 18 : 10
10 ikiwa watatenda maovu mbele za macho yangu, wasiitii sauti yangu, basi nitaghairi, nisitende mema yale niliyoazimia kuwatendea.

Yeremia 26 : 3
3 ⑤ Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu njia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya matendo yao maovu.

Yeremia 42 : 10
10 ⑫ Ikiwa mtabaki katika nchi hii, ndipo nitawajenga, wala sitawabomoa, nami nitawapanda, wala sitawang’oa; kwa maana nayajutia mabaya niliyowatenda.

Yoeli 2 : 13
13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi kuadhibu.

Amosi 7 : 3
3 BWANA akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema BWANA.

Amosi 7 : 6
6 BWANA akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU.

Yona 3 : 10
10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.

Mathayo 4 : 17
17 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Marko 1 : 15
15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.

Mithali 1 : 33
33 Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *