Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Tirza
Hesabu 26 : 33
33 ④ Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na watoto wa kiume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Nuhu, na Hogla, na Milka, na Tirza.
Hesabu 36 : 11
11 ⑫ kwa kuwa Mala, na Tirza, na Hogla, na Milka, na Nuhu, binti za Selofehadi waliolewa na wanaume, wana wa ndugu za baba yao.
Yoshua 17 : 3
3 Lakini Selofehadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, hakuwa na wana wa kiume ila binti; na majina ya hao binti zake walikuwa wakiitwa Mala, Nuhu, Hogla, Milka na Tirza.
Hesabu 27 : 11
11 Tena ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana wa Israeli, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Hesabu 36 : 13
13 ⑬ Haya ndiyo maagizo na hukumu, ambayo BWANA aliwaagiza wana wa Israeli, kwa mkono wa Musa, hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.
Yoshua 17 : 4
4 Nao wakaja mbele ya kuhani Eleazari, kuhani, na mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, na mbele ya viongozi, wakasema, BWANA alimwamuru Musa kutupa sisi urithi kati ya ndugu zetu; basi kwa kuifuata hiyo amri ya BWANA akawapa urithi kati ya ndugu za baba yao.
Yoshua 12 : 24
24 na mfalme wa Tirza, mmoja; wafalme hao wote walikuwa ni thelathini na mmoja.
1 Wafalme 14 : 17
17 Basi mkewe Yeroboamu akaondoka, akaenda zake, akafika Tirza; naye alipofika kizingitini kwa nyumba, huyo kijana akafa.
1 Wafalme 15 : 21
21 Ikawa Baasha aliposikia habari hiyo akaacha kuujenga Rama, akaenda akakaa Tirza.
1 Wafalme 15 : 33
33 Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya alianza kutawala juu ya Israeli wote huko Tirza, akatawala miaka ishirini na minne.
1 Wafalme 16 : 6
6 Baasha akalala na babaze, akazikwa katika Tirza; naye Ela mwanawe akatawala mahali pake.
1 Wafalme 16 : 9
9 Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamlia njama; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza;
1 Wafalme 16 : 15
15 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala muda wa siku saba huko Tirza. Basi, watu walikuwa wametua kambini kupigana na Gibethoni, ulio wa Wafilisti.
1 Wafalme 16 : 17
17 Omri akapanda kutoka Gibethoni, na Israeli wote pamoja naye, wakauhusuru Tirza.
1 Wafalme 16 : 23
23 Katika mwaka wa thelathini na moja wa Asa, mfalme wa Yuda, Omri alianza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka kumi na miwili. Akatawala huko Tirza miaka sita.
1 Wafalme 16 : 24
24 Kisha akanunua kilima cha Samaria kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha; akajenga juu ya kilima kile, akauita mji alioujenga Samaria, kwa kufuata jina lake Shemeri, aliyekuwa mwenye kilima.
2 Wafalme 15 : 14
14 Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza, akaja Samaria, akampiga Shalumu mwana wa Yabeshi huko Samaria, akamwua, akatawala mahali pake.
2 Wafalme 15 : 16
16 Ndipo Menahemu akapiga Tifsa, na wote waliokuwamo, na mipaka yake, toka Tirza; kwa sababu hawakumfungulia, kwa hiyo akaupiga; nao wanawake wote waliokuwamo wenye mimba akawapasua.
Leave a Reply