Biblia inasema nini kuhusu Tiglath-Pileser – Mistari yote ya Biblia kuhusu Tiglath-Pileser

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Tiglath-Pileser

2 Wafalme 15 : 29
29 Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.

1 Mambo ya Nyakati 5 : 6
6 na mwanawe huyo ni Beera, ambaye Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, alimchukua mateka; ndiye aliyekuwa mkuu wa Wareubeni.

1 Mambo ya Nyakati 5 : 26
26 Naye Mungu wa Israeli akamwamsha roho Pulu, mfalme wa Ashuru, yaani roho ya Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, naye akawachukua mateka hao Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila ya Wamanase; akawaleta mpaka Hala, na Habori, na Hara, na mpaka mto wa Gozani, hata siku hii ya leo.

2 Wafalme 16 : 10
10 Naye mfalme Ahazi akaenda Dameski ili aonane na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akaiona ile madhabahu iliyokuwako Dameski. Mfalme Ahazi akamletea Uria kuhani namna yake ile madhabahu, na cheo chake, kama ilivyokuwa kazi yake yote.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 21
21 Kwa maana Ahazi alitwaa sehemu katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme, na ya wakuu, akampa mfalme wa Ashuru; asisaidiwe na jambo hilo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *