Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Teman
Mwanzo 36 : 11
11 Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi.
Mwanzo 36 : 15
15 Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi,
Mwanzo 36 : 42
42 jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibsari,
1 Mambo ya Nyakati 1 : 36
36 Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 53
53 na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari;
Mwanzo 36 : 34
34 Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake.
Ayubu 2 : 11
11 Basi ikawa hao marafiki watatu wa Ayubu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumfariji Ayubu na kumtuliza moyo.
Yeremia 49 : 7
7 Kuhusu Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hakuna tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao?
Ezekieli 25 : 13
13 kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Nitanyosha mkono wangu juu ya Edomu, nitakatilia mbali nayo wanadamu na wanyama; nami nitaifanya kuwa ukiwa toka Temani; na mpaka Dedani wataanguka kwa upanga.
Amosi 1 : 12
12 lakini nitatuma moto juu ya Temani, nao utayateketeza majumba ya Bosra.
Obadia 1 : 9
9 Na mashujaa wako, Ee Temani, watafadhaika, hata iwe kila mtu akatiliwe mbali kwa kuuawa katika kilima cha Esau.
Habakuki 3 : 3
3 Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
Leave a Reply