Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia tamaa
Mathayo 5 : 28
28 ⑯ lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Wagalatia 5 : 16
16 Basi nasema, Nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
1 Wakorintho 6 : 18
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
1 Wathesalonike 4 : 3 – 5
3 ⑧ Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
4 ⑩ kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
5 ⑪ si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.
Wakolosai 3 : 5
5 Basi, viueni viungo vyenu vilivyo vya kidunia, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;
1 Yohana 2 : 16
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
2 Timotheo 2 : 22
22 ④ Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Wagalatia 5 : 19 – 21
19 ⑬ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi,
21 ⑭ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
1 Wakorintho 6 : 13
13 ⑭ Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.
Ayubu 31 : 1
1 Nilifanya agano na macho yangu; Basi ningewezaje kumwangalia msichana?
Warumi 8 : 6
6 ⑲ Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
Wagalatia 6 : 8
8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Yohana 14 : 15
15 ⑬ Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
1 Petro 2 : 11
11 ⑩ Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
Yakobo 1 : 14 – 15
14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
Waraka kwa Waebrania 13 : 4
4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Zaburi 119 : 37
37 Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako.
Wafilipi 4 : 8
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Zaburi 119 : 9 – 10
9 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
10 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
Leave a Reply