Biblia inasema nini kuhusu Talmai – Mistari yote ya Biblia kuhusu Talmai

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Talmai

Hesabu 13 : 22
22 ⑱ Wakapanda katika Negebu, wakafika Hebroni; na Ahimani, na Sheshai, na Talmai, wana wa Anaki, walikuwako huko. Nao Hebroni ulijengwa miaka saba kabla ya Soani wa Misri.

Yoshua 15 : 14
14 Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wazawa wa Anaki.

Waamuzi 1 : 10
10 Kisha Yuda akawafuatia hao Wakanaani waliokaa katika Hebroni; (jina la Hebroni hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Kiriath-arba;) nao wakamwua Sheshai, na Ahimani, na Talmai.

2 Samweli 3 : 3
3 ⑫ na wa pili wake Danieli, wa Abigaili mkewe Nabali wa Karmeli; na wa tatu Absalomu, mwana wa Maaka binti Talmai, mfalme wa Geshuri,

2 Samweli 13 : 37
37 Lakini Absalomu akakimbia, akamwendea Talmai, mwana wa Amihudi, mfalme wa Geshuri. Naye Daudi akamlilia mwanawe kila siku.

1 Mambo ya Nyakati 3 : 2
2 wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *