Biblia inasema nini kuhusu taji – Mistari yote ya Biblia kuhusu taji

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia taji

2 Timotheo 4 : 8
8 baada ya hayo nimewekewa taji la haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

Ufunuo 2 : 10
10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima.

Yakobo 1 : 12
12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Ufunuo 6 : 2
2 ⑤ Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, huku akishinda tena apate kushinda.

Zaburi 21 : 3
3 Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji la dhahabu safi kichwani pake.

Ufunuo 4 : 4
4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti niliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wameikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji la dhahabu.

Isaya 62 : 3
3 Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.

Ufunuo 4 : 10
10 ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao hutupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,

Ufunuo 3 : 11
11 ⑲ Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.

1 Wakorintho 9 : 25
25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo ili wapokee taji liharibikayo; bali sisi tupokee taji lisiloharibika.

Yohana 19 : 5
5 Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa lile taji la miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu!

Ufunuo 12 : 1
1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji la nyota kumi na mbili.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *