Biblia inasema nini kuhusu Taji – Mistari yote ya Biblia kuhusu Taji

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Taji

Kutoka 29 : 6
6 nawe mvike kile kilemba kichwani, na lile taji takatifu utalitia katika kile kilemba.

Kutoka 39 : 30
30 ⑲ Nao wakafanya hilo bamba la hilo taji takatifu la dhahabu safi, na kuandika juu yake andiko, mfano wa kuchorwa kwa mhuri, MTAKATIFU KWA BWANA.

Mambo ya Walawi 8 : 9
9 Akamvika na kile kilemba kichwani mwake; na juu ya kilemba, upande wa mbele, akakitia kile kipande cha dhahabu, hilo taji takatifu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.

2 Samweli 1 : 10
10 Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nilijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikalitwaa lile taji lililokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.

2 Samweli 12 : 30
30 ⑪ Kisha akamnyang’anya mfalme wao taji toka kichwani pake; na uzani wake ulikuwa talanta ya dhahabu, nalo lilikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani. Akazitoa nyara za huo mji, nyingi sana.

2 Wafalme 11 : 12
12 Ndipo akamleta nje mwana wa mfalme, akamvika taji, na kumpa ushuhuda; wakamfanya mfalme, wakamtia mafuta; wakapiga makofi, wakasema, Mfalme na aishi.

Esta 6 : 8
8 na aletewe mavazi ya kifalme ambayo mfalme amezoea kuyavaa, na farasi ambaye mfalme humpanda mwenyewe, ambaye ametiwa taji la kifalme kichwani;

Wimbo ulio Bora 3 : 11
11 Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alilovikwa na mamaye, Siku ya posa yake, Siku ya furaha ya moyo wake.

Ufunuo 6 : 2
2 ⑤ Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, huku akishinda tena apate kushinda.

Esta 1 : 11
11 wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, akiwa amevaa taji la kifalme; ili kuwaonesha watu na wakuu uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso.

Esta 2 : 17
17 Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji la kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti.

Esta 8 : 15
15 ② Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawati na nyeupe, mwenye taji kubwa la dhahabu, na joho la kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Susa wakapaza sauti, wakashangilia.

Zaburi 21 : 3
3 Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji la dhahabu safi kichwani pake.

Zekaria 6 : 11
11 naam, pokea fedha na dhahabu, ukatengeneze taji, ukamvike kichwani Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu;

2 Timotheo 2 : 5
5 Hata mwanariadha hapewi taji, asiposhindana kwa kufuata sheria.

Ezekieli 23 : 42
42 Na sauti za wingi wa watu wenye hali ya raha zilikuwa pamoja naye; na pamoja na watu wasio na adabu, waliletwa walevi toka jangwani; wakawatia vikuku mikononi, na taji zuri juu ya vichwa vyao.

Ezekieli 16 : 12
12 Nikatia kishaufu puani mwako, na herini masikioni mwako, na taji zuri juu ya kichwa chako.

2 Samweli 12 : 30
30 ⑪ Kisha akamnyang’anya mfalme wao taji toka kichwani pake; na uzani wake ulikuwa talanta ya dhahabu, nalo lilikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani. Akazitoa nyara za huo mji, nyingi sana.

1 Mambo ya Nyakati 20 : 2
2 Kisha Daudi akatwaa taji la Milkomu[13] toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana.

Zekaria 9 : 16
16 ⑯ Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimetameta juu ya nchi yake.

Isaya 62 : 3
3 Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.

Mathayo 27 : 29
29 Wakasokota taji la miiba, wakaliweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kulia; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!

Marko 15 : 17
17 Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji la miiba, wakamtia kichwani;

Yohana 19 : 5
5 Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa lile taji la miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu!

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *