Biblia inasema nini kuhusu Tabor – Mistari yote ya Biblia kuhusu Tabor

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Tabor

Yoshua 19 : 22
22 ⑪ na mpaka ukafikia hadi Tabori, na Shahasuma na Beth-shemeshi; na mwisho wa mpaka wao ulikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

Waamuzi 8 : 18
18 Ndipo akawaambia hao Zeba na Salmuna, Hao watu mliowaua huko Tabori walikuwa watu wa namna gani? Wakamjibu, Walikuwa kama wewe ulivyo; kila mmoja alikuwa anafanana na wana wa mfalme.

Zaburi 89 : 12
12 Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba, Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.

Yeremia 46 : 18
18 ⑲ Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja.

Hosea 5 : 1
1 Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.

Waamuzi 4 : 6
6 Siku moja Debora akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu kutoka Kedesh-Naftali, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli anakuamuru hivi: “Nenda, ukawaogoze watu elfu kumi na wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni, ili washike doria katika mlima Tabori”.

Waamuzi 4 : 12
12 Watu wakamwambia Sisera ya kwamba Baraka, mwana wa Abinoamu amekwea kwenda mlima wa Tabori.

Waamuzi 4 : 14
14 Debora akamwambia Baraka, Haya! Inuka; maana siku hii ndiyo siku ambayo BWANA amemtia Sisera katika mkono wako. Je! BWANA hakutoka atangulie mbele yako? Basi Baraka akashuka katika mlima wa Tabori, na watu elfu kumi wakamfuata.

1 Samweli 10 : 3
3 ⑤ Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwenye mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *