Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sukoti
Mwanzo 33 : 17
17 Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi.
Yoshua 13 : 27
27 ⑤ tena katika bonde, Beth-haramu, na Bethnimira, na Sukothi, na Safoni, hiyo iliyosalia ya ufalme wa Sihoni mfalme wa Heshboni, yaani mto wa Yordani na kingo zake, mpaka mwisho wa bahari ya Kinerethi ng’ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki.
Waamuzi 8 : 8
8 Basi kutoka hapo alikwea kwenda Penieli, akasema na watu wa mahali hapo maneno kama hayo; watu wa Penieli nao wakamjibu kama vile watu wa Sukothi walivyomjibu.
Waamuzi 8 : 16
16 Basi akawatwaa hao wazee wa mji, na miiba ya nyikani na michongoma, akawafunza hao watu wa Sukothi kwayo.
1 Wafalme 7 : 46
46 ⑰ Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sarethani.
2 Mambo ya Nyakati 4 : 17
17 Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda.
Zaburi 60 : 6
6 ⑯ Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nikishangilia. Nitaigawanya Shekemu, Na kulipima bonde la Sukothi.
Zaburi 108 : 7
7 Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nitashangilia. Nitaigawanya Shekemu, Nitalipima bonde la Sukothi.
Kutoka 12 : 37
37 ⑰ Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu elfu mia sita wanaume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto.
Kutoka 13 : 20
20 Nao wakasafiri kutoka Sukothi, wakapiga kambi Ethamu, kwenye mpaka wa lile jangwa.
Hesabu 33 : 6
6 Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapiga kambi Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika.
Leave a Reply