Biblia inasema nini kuhusu Sinai – Mistari yote ya Biblia kuhusu Sinai

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sinai

Kutoka 16 : 1
1 Kisha wakasafiri kutoka Elimu, na mkutano wote wa wana wa Israeli wakafikia jangwa la Sini, lililoko kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri.

Kutoka 19 : 2
2 Nao walipokuwa wameondoka Refidimu na kufika jangwa la Sinai, wakatua katika lile jangwa; Israeli wakapiga kambi huko wakiukabili mlima.

Kumbukumbu la Torati 1 : 2
2 Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya mlima wa Seiri mpaka Kadesh-barnea.

Kutoka 19 : 25
25 Basi Musa akawateremkia hao watu na kuwaambia hayo.

Kutoka 24 : 18
18 Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arubaini, mchana na usiku.

Kutoka 32 : 16
16 Na zile mbao zilikuwa kazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa katika zile mbao.

Kutoka 34 : 4
4 Naye akachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza; na Musa akainuka na mapema asubuhi, naye akakwea katika mlima wa Sinai, kama BWANA alivyomwamuru, akazichukua hizo mbao mbili za mawe mkononi mwake.

Mambo ya Walawi 7 : 38
38 ambazo BWANA alimwagiza Musa katika mlima wa Sinai, siku hiyo aliyowaagiza wana wa Israeli wamtolee BWANA matoleo yao, huko katika jangwa la Sinai.

Mambo ya Walawi 25 : 1
1 ③ Kisha BWANA akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia,

Mambo ya Walawi 26 : 46
46 ⑰ Hizi ni amri, maagizo na sheria, BWANA alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.

Mambo ya Walawi 27 : 34
34 Haya ndiyo maagizo, BWANA aliyomwagiza Musa kwa ajili ya wana wa Israeli katika mlima wa Sinai.

Hesabu 3 : 1
1 Basi vizazi vya Haruni na Musa, siku hiyo BWANA aliyosema na Musa katika mlima wa Sinai, ni hivi.

Kumbukumbu la Torati 4 : 15
15 ⑯ Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yoyote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;

Kumbukumbu la Torati 5 : 26
26 ⑮ Maana katika watu wote ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka kati ya moto, kama vile sisi, asife?

Kumbukumbu la Torati 29 : 1
1 Haya ndiyo maneno ya agano BWANA alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.

Kumbukumbu la Torati 33 : 2
2 ⑬ Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawajia kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kulia Palikuwa na sheria ya motomoto kwao.

Nehemia 9 : 13
13 ⑤ Tena ulishuka juu ya mlima Sinai, ukasema nao toka mbinguni, ukawapa hukumu za haki, na sheria za kweli, na amri nzuri na maagizo;

Zaburi 68 : 8
8 Nchi ilitetemeka Naam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu; Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.

Zaburi 68 : 17
17 Magari ya Mungu ni elfu ishirini, maelfu kwa maelfu; Bwana yumo kati yao kama katika Sinai, Katika patakatifu.

Malaki 4 : 4
4 ⑫ Ikumbukeni Torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.

Matendo 7 : 30
30 Hata miaka arubaini ilipotimia, malaika wa Bwana akamtokea katika jangwa la mlima wa Sinai katika muali wa moto, kichakani.

Matendo 7 : 38
38 Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima ili atupe sisi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *