Biblia inasema nini kuhusu Sila – Mistari yote ya Biblia kuhusu Sila

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sila

Matendo 15 : 34
34 Lakini Sila akaona vema kukaa huko.]

Matendo 15 : 41
41 Akapita katika Shamu na Kilikia akiyaimarisha makanisa.

2 Wakorintho 1 : 19
19 Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na Siyo; bali katika yeye ni Ndiyo.

1 Wathesalonike 1 : 1
1 Paulo, Silwano na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.

2 Wathesalonike 1 : 1
1 Paulo, Silwano na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo.

Matendo 16 : 40
40 Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Lidia; na walipokwisha kuonana na ndugu wakawafariji, wakaenda zao.

Matendo 17 : 10
10 Mara hao ndugu wakawatuma Paulo na Sila usiku hadi Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi.

Matendo 17 : 14
14 ⑪ Mara hiyo wale ndugu wakamtuma Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakabakia huko.

Matendo 17 : 15
15 Lakini wale waliomsindikiza Paulo wakampeleka mpaka Athene; nao wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kwamba wasikawie kumfuata, wakaenda zao.

Matendo 18 : 5
5 Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.

1 Petro 5 : 12
12 Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nijuavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika hiyo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *