Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia sikukuu za kipagani
Yeremia 10 : 1 – 4
1 Enyi nyumba ya Israeli, lisikieni neno awaambialo BWANA;
2 ⑳ BWANA asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo.
3 Maana desturi za watu hao ni ubatili, maana mtu mmoja hukata mti mwituni, kazi ya mikono ya fundi na shoka.
4 Huupamba kwa fedha na dhahabu; huukaza kwa misumari na nyundo, usitikisike.
Yohana 8 : 32
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Wakolosai 2 : 8
8 ⑩ Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
1 Wakorintho 11 : 1 – 2
1 ⑤ Mniige mimi kama mimi ninavyomwiga Kristo.
2 Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.
1 Wakorintho 5 : 6 – 8
6 ① Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima?
7 ② Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;
8 ③ basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.
2 Timotheo 2 : 15
15 Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.
Yohana 6 : 50 – 71
50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.
51 ⑥ Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.
52 ⑦ Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?
53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56 ⑧ Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.
57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.
58 Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.
59 Maneno hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha, huko Kapernaumu.
60 Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia?
61 Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza?
62 ⑩ Itakuwaje basi, mumwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza?
63 ⑪ Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
64 ⑫ Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti.
65 ⑬ Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.
66 Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.
67 Basi Yesu akawaambia wale Kumi na Wawili, Je! Ninyi nanyi mnataka kuondoka?
68 ⑭ Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
69 ⑮ Nasi tumeamini, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.
70 Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Kumi na Wawili, na mmoja wenu ni shetani?
71 Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Kumi na Wawili.
Wagalatia 4 : 9
9 Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena?
Wakolosai 2 : 16
16 ⑱ Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
Leave a Reply