Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia siku za kuzaliwa
Mhubiri 7 : 1
1 Heri sifa njema kuliko manukato ya thamani; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.
Mathayo 14 : 6
6 Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.
Kumbukumbu la Torati 30 : 15 โ 20
15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;
16 kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.
17 Lakini moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikiza, lakini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia;
18 โ nawahubiria hivi leo hakika mtaangamia; hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukiayo Yordani, uingie kuimiliki.
19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
20 โก kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.
Mwanzo 40 : 20
20 โฑ Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.
Marko 6 : 21
21 Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya;
Ayubu 1 : 4
4 Nao wanawe wa kiume huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakawaalika dada zao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao.
Leave a Reply