Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia siku ya kuzaliwa
Hesabu 6 : 24 – 26
24 ⑪ BWANA akubariki, na kukulinda;
25 ⑫ BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;
26 ⑬ BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.
Mithali 9 : 11
11 ④ Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa.
Yakobo 1 : 17
17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Zaburi 91 : 11
11 Kwa kuwa atakuagizia malaika wake Wakulinde katika njia zako zote.
Zaburi 118 : 24
24 Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA, Tutashangilia na kuifurahia.
Zaburi 65 : 11
11 ④ Umeuvika mwaka taji la wema wako; Mapito yako yadondoza unono.
2 Wakorintho 9 : 15
15 Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo.
Mhubiri 7 : 1
1 Heri sifa njema kuliko manukato ya thamani; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.
1 Wakorintho 1 : 3 – 7
3 Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
4 Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu;
5 kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote;
6 kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu;
7 hata hamkupungukiwa na karama yoyote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;
Wagalatia 6 : 9
9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.
Yakobo 2 : 18
18 ③ Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
Habakuki 3 : 2
2 Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.
2 Wakorintho 8 : 9
9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Mithali 8 : 20 – 21
20 Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu.
21 Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao.
Warumi 5 : 5
5 ⑱ na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.
Waefeso 2 : 8 – 9
8 ③ Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9 ④ wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Matendo 2 : 25 – 28
25 ⑥ Maana Daudi ataja habari zake, Nilimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kulia, nisitikisike.
26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.
27 ⑦ Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.
28 Umenijulisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako.
Zaburi 90 : 12
12 ⑯ Basi, utufundishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.
Wakolosai 1 : 13 – 16
13 Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa;
14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.
15 Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au milki, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Mathayo 11 : 11
11 Lakini, nawaambieni, Hajatokea mtu katika wazawa wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.
Leave a Reply