Biblia inasema nini kuhusu Siku – Mistari yote ya Biblia kuhusu Siku

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Siku

Mwanzo 1 : 5
5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

Mwanzo 1 : 8
8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.

Mwanzo 1 : 13
13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.

Mwanzo 1 : 19
19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.

Mwanzo 1 : 23
23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.

Mwanzo 1 : 31
31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.

Mwanzo 2 : 2
2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

Yohana 11 : 9
9 ⑧ Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

2 Petro 3 : 8
8 ⑮ Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.

Danieli 8 : 14
14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.

Danieli 9 : 27
27 ① Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.

Danieli 12 : 12
12 Heri angojaye, na kuzifikia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano.

Ufunuo 11 : 3
3 Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, wakiwa wamevikwa magunia.

Ufunuo 9 : 15
15 ⑤ Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.

Ufunuo 12 : 6
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.

Kutoka 20 : 9
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;

Ezekieli 46 : 1
1 ⑱ Bwana MUNGU asema hivi; Lango la ua wa ndani, lielekealo upande wa mashariki litafungwa siku sita za kazi; lakini siku ya sabato litafunguliwa, na siku ya mwezi mwandamo litafunguliwa.

Marko 15 : 42
42 Ilipofika wakati wa jioni, kwa sababu ni Maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya sabato,

Yohana 19 : 14
14 Nayo ilikuwa Maandalio ya Pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!

Yohana 19 : 31
31 Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe.

Yohana 19 : 42
42 Humo basi, kwa sababu ya Maandalio ya Wayahudi, wakamweka Yesu; maana lile kaburi lilikuwa karibu.

Ufunuo 1 : 10
10 Nilikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *