Biblia inasema nini kuhusu Sikio – Mistari yote ya Biblia kuhusu Sikio

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sikio

Kutoka 29 : 20
20 Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Haruni la upande wa kulia, na katika ncha za masikio ya kulia ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kulia, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kandokando.

Mambo ya Walawi 8 : 23
23 ① Kisha akamchinja; na Musa akatwaa baadhi ya damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la Haruni, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole cha gumba cha guu lake la kulia.

Mambo ya Walawi 14 : 14
14 ⑧ kisha huyo kuhani atatwaa baadhi ya hiyo damu ya sadaka ya hatia, naye kuhani ataitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;

Mambo ya Walawi 14 : 25
25 ⑭ kisha atamchinja mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na kuhani atatwaa katika damu ya sadaka ya hatia, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;

Mambo ya Walawi 14 : 17
17 ⑩ na katika yale mafuta yaliyobaki mkononi mwake kuhani atayatia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia, juu ya damu ya sadaka ya hatia;

Mambo ya Walawi 14 : 28
28 ⑮ kisha kuhani atatia mengine katika hayo mafuta yaliyo mkononi mwake katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia, juu ya mahali pale penye damu ya sadaka ya hatia;

Kutoka 21 : 6
6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote.

Zaburi 17 : 6
6 Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu.

Zaburi 39 : 12
12 ⑫ Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyapuuze machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.

Zaburi 77 : 1
1 Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.

Zaburi 80 : 1
1 Wewe uchungaye Israeli, usikie, Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi; Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.

Zaburi 84 : 8
8 BWANA, Mungu wa majeshi, uyasikie maombi yangu, Ee Mungu wa Yakobo, usikilize, wako.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *