Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Siki
Hesabu 6 : 3
3 atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yoyote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka.
Ruthu 2 : 14
14 Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza.
Zaburi 69 : 21
21 Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Na nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.
Mithali 10 : 26
26 Kama siki menoni, na kama moshi machoni, Ndivyo alivyo mtu mvivu kwa hao waliomwajiri.
Mithali 25 : 20
20 ⑱ Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito, Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi; Ni kama siki juu ya magadi.
Mathayo 27 : 34
34 ④ wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.
Mathayo 27 : 48
48 ⑫ Mara mmoja wao akaenda mbio, akatwaa sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha.
Yohana 19 : 29
29 Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani.
Marko 15 : 23
23 Wakampa mvinyo iliyotiwa manemane, asiipokee.
Leave a Reply