Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sidoni
Mwanzo 10 : 15
15 Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
1 Mambo ya Nyakati 1 : 13
13 Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi;
Mwanzo 10 : 19
19 ⑬ Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.
Mwanzo 49 : 13
13 Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
Yoshua 19 : 28
28 ⑮ na Ebroni, Rehobu, Hamoni, Kana, hadi kufikia Sidoni Kuu;
2 Samweli 24 : 6
6 kisha wakaja Gileadi, na nchi ya Wahiti huko Kadeshi; kisha wakaja Dani, na kutoka Dani wakazunguka mpaka Sidoni,
Yoshua 13 : 6
6 na watu wote wenye kukaa nchi za vilima kutoka Lebanoni hadi Misrefoth-maimu, maana, hao Wasidoni wote; hao wote nitawafukuza watoke mbele ya wana wa Israeli; lakini wewe uwape Israeli kuwa ni urithi wao, kama nilivyokuamuru.
Waamuzi 18 : 7
7 Ndipo hao watu watano wakaenda zao, wakafika Laisha, wakawaona wale watu waliokuwamo ndani yake, jinsi walivyokaa kwa amani, kama ilivyokuwa desturi ya Wasidoni, watu watulivu na wasioshuku, wasiopungukiwa[15] na chochote duniani, na waliokuwa na miliki;[16] Nao walikuwa mbali na hao Wasidoni, wala hawakutangamana na watu wengine.
Waamuzi 1 : 31
31 Asheri naye hakuwatoa wenyeji wa Aka, wala hao waliokaa Sidoni, wala hao wa Alabu, wala hao wa Akzibu, wala hao wa Helba, wala hao wa Afeka, wala hao wa Rehobu;
Waamuzi 3 : 3
3 ⑱ aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi.
1 Wafalme 5 : 6
6 Basi uamuru wanikatie mierezi ya Lebanoni; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni.
1 Mambo ya Nyakati 22 : 4
4 ⑧ na mierezi isiyo na idadi; kwa kuwa Wasidoni na watu wa Tiro walimletea Daudi mierezi tele.
Ezra 3 : 7
7 ⑥ Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete mierezi kutoka Lebanoni mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi.
Leave a Reply