Biblia inasema nini kuhusu Siagi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Siagi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Siagi

Mwanzo 18 : 8
8 Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandalia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.

Kumbukumbu la Torati 32 : 14
14 Siagi ya ng’ombe, na maziwa ya kondoo, Pamoja na mafuta ya wana-kondoo, Kondoo dume wa Kibashani, na mbuzi, Na unono wa ngano iliyo nzuri; Ukanywa divai, damu ya mizabibu.

Waamuzi 5 : 25
25 Aliomba maji, naye akampa maziwa. Akamletea siagi katika sahani ya heshima.

2 Samweli 17 : 29
29 ⑮ na asali, na siagi, na kondoo, na samli ya ng’ombe, wapate kula Daudi na watu waliokuwa pamoja naye; kwani walisema, Watu hao wanaona njaa, tena wamechoka, nao wana kiu huku nyikani.

Ayubu 20 : 17
17 ⑭ Hataiangalia hiyo mito ya maji, Vile vijito vilivyojaa asali na siagi.

Isaya 7 : 15
15 Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema.

Isaya 7 : 22
22 kisha itakuwa, kwa sababu wanyama hao watatoa maziwa mengi, atakula siagi; kwa maana kila mtu aliyesalia katika nchi hii atakula siagi na asali.

Mithali 30 : 33
33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *