Biblia inasema nini kuhusu Shule – Mistari yote ya Biblia kuhusu Shule

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shule

1 Samweli 19 : 20
20 ⑦ Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, Roho ya Mungu ikawajia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.

2 Wafalme 2 : 3
3 Elisha akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha, Basi wakashuka mpaka Betheli. Basi wana wa manabii, waliokuwako Betheli, wakatoka kuonana na Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akasema, Naam, najua; nyamazeni.

2 Wafalme 2 : 5
5 Basi wana wa manabii, waliokuwako Yeriko, wakamkaribia Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akajibu, Naam, najua, nyamazeni.

2 Wafalme 2 : 15
15 Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.

2 Wafalme 4 : 38
38 Elisha akafika Gilgali tena; na kulikuwa na njaa katika nchi; na hao wana wa manabii walikuwa wakikaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, Teleka sufuria kubwa, uwapikie wana wa manabii.

2 Wafalme 22 : 14
14 Basi Hilkia kuhani, na Ahikamu, na Akbori, na Shafani, na Asaya, wakamwendea Hulda, nabii wa kike, mkewe Shalumu, mwana wa Tikva, mwana wa Harhasi, mtunza mavazi ya mfalme; (naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili;) wakasema naye.

2 Mambo ya Nyakati 34 : 22
22 ⑰ Basi Hilkia, na hao waliotumwa na mfalme, wakamwendea Hulda, nabii mwanamke, mkewe Shalumu, mwana wa Tohathi, mwana wa Hasra, mtunza mavazi; (naye alikuwa akikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili); wakasema naye kama hayo.

2 Wafalme 6 : 1
1 ⑯ Kisha, wana wa manabii wakamwambia Elisha, Angalia basi, mahali tukaapo mbele yako ni padogo kwetu.

Kumbukumbu la Torati 4 : 10
10 ⑪ siku ile uliyosimama mbele za BWANA wako huko Horebu, BWANA aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawafanya wasikilize maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao.

Kumbukumbu la Torati 6 : 7
7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

Kumbukumbu la Torati 6 : 9
9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

Kumbukumbu la Torati 11 : 20
20 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako;

Zaburi 78 : 8
8 Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.

Kumbukumbu la Torati 31 : 13
13 ⑮ na watoto wao wasiojua, wapate kusikia na kujifunza kumcha BWANA, Mungu wenu, siku zote mtakazokaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki.

2 Mambo ya Nyakati 17 : 9
9 ⑩ Wakafundisha katika Yuda, wenye kitabu cha Torati ya BWANA; wakazunguka katika miji yote ya Yuda, wakafundisha kati ya watu.

Danieli 1 : 21
21 Tena, Danieli huyo akadumu huko hata mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi.

Matendo 5 : 34
34 Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo kidogo,

Matendo 22 : 3
3 ⑧ Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nilizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihada kubwa kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; ⑩

Matendo 19 : 9
9 Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika darasa la mtu mmoja, jina lake Tirano.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *