Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shoka
Kumbukumbu la Torati 19 : 5
5 kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai;
1 Samweli 13 : 21
21 Na walilipa theluthi mbili za shekeli kunoa jembe na miundu, na theluthi moja ya shekeli kunoa mashoka na kuchonga michokoo.
2 Samweli 12 : 31
31 Naye akawatoa watu waliokuwamo, akawaweka kwenye kazi ya[10] misumeno, na sululu za chuma, na mashoka ya chuma, akawafanyiza kazi tanurini mwa matofali; ndivyo alivyoifanya miji yote ya wana wa Amoni. Kisha Daudi akarudi na watu wote Yerusalemu.
Zaburi 74 : 6
6 Na sasa nakishi yake yote pia Wanaivunjavunja kwa mashoka na nyundo.
2 Wafalme 6 : 6
6 ⑰ Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea.
Ezekieli 26 : 9
9 Naye ataweka vyombo vyake vya kubomolea mbele za kuta zako, na kwa mashoka yake ataiangusha chini minara yako.
Yeremia 46 : 22
22 Sauti yake ni kama nyoka, wajapo kwa nguvu, Watamjia na mashoka, kama wachanja kuni.
Yeremia 51 : 20
20 ⑮ Wewe ni rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;
Mathayo 3 : 10
10 ⑩ Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
Leave a Reply