Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shelomithi
Mambo ya Walawi 24 : 11
11 kisha huyo mwanamume ambaye mama ni Mwisraeli akakufuru jina la Bwana na kulaani nao watu wakampeleka kwa Musa. Mama yake mtu huyo alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila la Dani.
1 Mambo ya Nyakati 3 : 19
19 Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa dada yao;
1 Mambo ya Nyakati 23 : 9
9 Wana wa Shimei; Shelomothi, na Hazieli, na Harani, watatu. Hao walikuwa vichwa vya koo za baba za Ladani.
1 Mambo ya Nyakati 23 : 18
18 Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao.
1 Mambo ya Nyakati 24 : 22
22 Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi.
1 Mambo ya Nyakati 26 : 26
26 Huyo Shelomothi na ndugu zake walikuwa wasimamizi wa hazina zote za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyoviweka wakfu mfalme Daudi, na hao wakuu wa koo za mababa, na maofisa wa maelfu na wa mamia, na makamanda wa jeshi.
1 Mambo ya Nyakati 26 : 28
28 Na vyote alivyoviweka wakfu Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, na Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya; na mtu yeyote aliyekiweka wakfu kitu chochote, kilikuwa chini ya mkono wa Shelomothi na nduguze.
2 Mambo ya Nyakati 11 : 20
20 Kisha baada yake akamwoa Maaka, binti Absalomu; na yeye akamzalia Abiya, na Atai, na Ziza, na Shelomithi.
Ezra 8 : 10
10 Na wa wana wa Binui, Shelomithi, mwana wa Yosifia; na pamoja naye wanaume mia moja na sitini.
Leave a Reply