Biblia inasema nini kuhusu Shela – Mistari yote ya Biblia kuhusu Shela

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shela

Mwanzo 38 : 5
5 Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwa huko Kezibu, alipomzaa.

Mwanzo 38 : 11
11 Yuda akamwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata Shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, Asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye.

Mwanzo 38 : 14
14 Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, ijapokuwa hakuozwa awe mkewe.

Mwanzo 38 : 26
26 Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo.

Mwanzo 46 : 12
12 Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli.

Hesabu 26 : 20
20 Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera.

1 Mambo ya Nyakati 2 : 3
3 Wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela; ambao hao watatu alizaliwa na binti Shua, Mkanaani. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; naye akamwua.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *