Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sheba
Mwanzo 10 : 7
7 Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 9
9 Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani.
Mwanzo 10 : 28
28 na Obali, na Abimaeli, na Seba,
1 Mambo ya Nyakati 1 : 22
22 na Obali, na Abimaeli, na Sheba;
Mwanzo 25 : 3
3 Yokshani akamzaa Sheba, na Dedani; na wana wa Dedani walikuwa Waashuri na Waletushi, na Waleumi.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 32
32 Na wana wa Ketura, suria yake Abrahamu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.
1 Mambo ya Nyakati 5 : 13
13 na ndugu zao wa koo za baba zao; Mikaeli, na Meshulamu, na Sheba, na Yorai, na Yakani, na Zia, na Eberi, watu saba.
Yoshua 19 : 2
2 ③ Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, Sheba, Molada;
1 Wafalme 10 : 13
13 Naye mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba haja yake yote, kila alilotaka, zaidi ya hayo aliyopewa na Sulemani kwa ukarimu wake wa kifalme. Basi, akarudi akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
2 Mambo ya Nyakati 9 : 12
12 Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichokitaka na zaidi ya vile alivyomletea mfalme. Basi akarudi, akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Zaburi 72 : 10
10 ⑳ Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
Zaburi 72 : 15
15 Na aishi maisha marefu! Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa.
Yeremia 6 : 20
20 ① Yafaa nini niletewe ubani kutoka Sheba, na udi kutoka nchi iliyo mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliwi, wala dhabihu zenu haziniridhii.
Ezekieli 27 : 23
23 ⑦ Harani, na Kane, na Adini, wachuuzi wa Sheba, na Ashuru, na Kilmadi, walikuwa wachuuzi wako.
Ezekieli 38 : 13
13 Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi, pamoja na wanasimba wake wote, watakuambia, Je! Umekuja kuteka mateka? Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua ng’ombe na mali, kuteka kiasi kikubwa cha nyara?
Leave a Reply