Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shauli
Mwanzo 46 : 10
10 Na wana wa Simeoni; Yemueli na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli, mwana wa mwanamke Mkanaani.
Kutoka 6 : 15
15 Na wana wa Simeoni; ni Yemueli, na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli mwana wa mwanamke wa Kikanaani; hao ni jamaa za Simeoni.
Hesabu 26 : 13
13 wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli.
1 Mambo ya Nyakati 4 : 24
24 Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli;
1 Mambo ya Nyakati 1 : 49
49 Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake.
Mwanzo 36 : 37
37 Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake.
1 Mambo ya Nyakati 6 : 24
24 na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Urieli, na mwanawe huyo ni Uzia, na mwanawe huyo ni Shauli.
Leave a Reply