Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shahidi wa Uongo
Kutoka 20 : 16
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
Kumbukumbu la Torati 5 : 20
20 ⑫ Wala usimshuhudie jirani yako uongo.
Mathayo 19 : 18
18 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo,
Luka 18 : 20
20 Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.
Warumi 13 : 9
9 ④ Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Kutoka 23 : 1
1 Usivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo.
Mambo ya Walawi 6 : 3
3 au kupata kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo;
Mambo ya Walawi 19 : 12
12 ⑯ Msiape uongo kwa jina langu, na ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.
Mambo ya Walawi 19 : 16
16 ⑳ Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidi kwa damu[9] ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.
Kumbukumbu la Torati 19 : 20
20 Na watakaosalia watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako.
Zaburi 27 : 12
12 Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wamenijia, Nao watoao jeuri kama pumzi.
Zaburi 35 : 11
11 Mashahidi wa udhalimu wanasimama, Wananiuliza mambo nisiyoyajua.
Mithali 6 : 19
19 ⑦ Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
Mithali 12 : 17
17 Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila.
Mithali 14 : 5
5 Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.
Mithali 14 : 8
8 Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
Mithali 14 : 25
25 Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu; Bali atoaye uongo hudanganya.
Mithali 18 : 5
5 Kukubali uso wake asiye haki si vizuri; Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.
Mithali 19 : 9
9 Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Naye asemaye uongo ataangamia.
Mithali 19 : 22
22 Haja ya mwanadamu ni hisani yake; Ni afadhali maskini kuliko mwongo.
Mithali 19 : 28
28 Shahidi asiyefaa kitu hudhihaki hukumu, Na vinywa vya wasio haki humeza uovu.
Mithali 21 : 28
28 Shahidi wa uongo atapotea; Bali mtu asikiaye atasema maneno yadumuyo.
Mithali 24 : 28
28 ⑥ Usimshuhudie jirani yako pasipo sababu, Wala usidanganye kwa midomo yako.
Mithali 25 : 18
18 ⑯ Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo Ni nyundo, na upanga, na mshale mkali.
Zekaria 5 : 4
4 ⑳ Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.
Mathayo 15 : 19
19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
Luka 3 : 14
14 Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.
Leave a Reply