Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sensa
Kutoka 38 : 26
26 ② kichwa beka, maana, nusu shekeli, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu, kwa ajili ya kila mtu aliyepita kwa wale waliohesabiwa, aliyekuwa wa umri wa miaka ishirini au zaidi, kwa ajili ya wanaume elfu mia sita na tatu mia tano na hamsini (603,550).
Hesabu 3 : 43
43 Wazaliwa wa kwanza wote walio wanaume kwa hesabu ya majina, kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi, katika hao waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu ishirini na mbili na mia mbili na sabini na watatu.
2 Samweli 24 : 9
9 Naye Yoabu akamtolea mfalme jumla ya hesabu ya watu; nao walikuwa wa Israeli mashujaa elfu mia nane wenye kufuta panga; nao wa Yuda walikuwa watu elfu mia tano.
1 Mambo ya Nyakati 21 : 8
8 Naye Daudi akamwambia Mungu, Nimekosa sana, kwa kuwa nimelifanya jambo hili; lakini sasa uuondolee mbali, nakusihi, uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa.
1 Mambo ya Nyakati 27 : 24
24 Yoabu, mwana wa Seruya, alianza kuwahesabu, lakini hakumaliza; na ghadhabu ikawapata Israeli kwa hayo; wala hesabu hiyo haikuingizwa katika kumbukumbu za mfalme Daudi.
Kutoka 30 : 16
16 Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
Kutoka 38 : 26
26 ② kichwa beka, maana, nusu shekeli, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu, kwa ajili ya kila mtu aliyepita kwa wale waliohesabiwa, aliyekuwa wa umri wa miaka ishirini au zaidi, kwa ajili ya wanaume elfu mia sita na tatu mia tano na hamsini (603,550).
Luka 2 : 3
3 Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao.
Leave a Reply