Biblia inasema nini kuhusu sayansi – Mistari yote ya Biblia kuhusu sayansi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia sayansi

Zaburi 111 : 2
2 ⑫ Matendo ya BWANA ni makuu, Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.

Ayubu 38 : 4 – 30
4 Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama una ufahamu.
5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake — hakika unajua! Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?
6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
7 ① Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
8 ② Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi.[6]
9 Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,
10 Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango,
11 Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yenye nguvu yatazuiliwa?
12 Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?
13 Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo?
14 Hubadilika mfano wa udongo chini ya mhuri, Vitu vyote vinatokea kama mavazi.
15 Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika.
16 Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi?
17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?
18 Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.
19 Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi?
20 Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuyaelewa mapito ya kuiendea nyumba yake?
21 Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, Na hesabu ya siku zako ni kubwa!
22 Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe,
23 ③ Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita?
24 Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi?
25 Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, Au njia kwa umeme wa radi;
26 Kunyesha mvua juu ya nchi isiyo na watu; Juu ya jangwa asiyokaa mwanadamu;
27 ④ Kuishibisha nchi iliyo kame na ukiwa, Na kuyameza majani yaliyo mororo?
28 ⑤ Je! Mvua ina baba? Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande?
29 ⑥ Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa?
30 Maji hugandamana kama jiwe, Na uso wa vilindi huganda kwa baridi.

Isaya 40 : 12
12 Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiria mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?

Zaburi 104 : 5
5 Uliiweka nchi juu ya misingi yake, Isitikisike milele.

Mwanzo 1 : 1
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Isaya 40 : 22
22 Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;

Mhubiri 1 : 6 – 7
6 Upepo huvuma kuelekea kusini, kisha huvuma kuelekea kaskazini; hugeuka daima katika mwendo wake, nao huyarudia mazunguko yake.
7 Mito yote huingia baharini, lakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.

Mhubiri 1 : 13 – 17
13 Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.
14 Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kufukuza upepo.[2]
15 Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki.
16 Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa.
17 Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kufukuza upepo.

1 Timotheo 6 : 20
20 ③ Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na mazungumzo yasiyo ya kimungu, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;

Ayubu 26 : 7
7 ⑯ Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.

Warumi 1 : 20
20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;

Ayubu 38 : 4
4 Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama una ufahamu.

Wakolosai 1 : 17
17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.

Mwanzo 1 : 27
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Ayubu 26 : 7 – 14
7 ⑯ Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.
8 ⑰ Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake.
9 Husitiri uso wa kiti chake cha enzi, Na kulitandaza wingu lake juu yake.
10 ⑱ Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.
11 Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake.
12 ⑲ Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake.
13 ⑳ Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.
14 Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong’ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa?

Mwanzo 1 : 1 – 31
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
2 Nayo nchi ilikuwa tupu, tena bila umbo, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.
7 Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.
9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.
14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili ya kuonesha majira, siku na miaka;
15 tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.
16 Mungu akaumba mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.
17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi
18 na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.
20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na viumbe vyenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
25 Mungu akaumba aina zote za wanyama wa porini na wa kufugwa na viumbe vyote vitambaavyo nchini; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mmea utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa chakula chenu;
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.

Mithali 8 : 27
27 Alipozithibitisha mbingu nilikuwako; Alipopiga duara katika uso wa bahari;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *