Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sauli
Mwanzo 36 : 38
38 Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 49
49 Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake.
1 Samweli 9 : 2
2 Naye alikuwa na mwana, aliyeitwa Sauli, kijana, tena mzuri; wala katika wana wa Israeli hakuwako mtu mzuri kuliko yeye; tangu mabega yake kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wote.
1 Mambo ya Nyakati 8 : 33
33 ⑲ Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.
1 Samweli 9 : 2
2 Naye alikuwa na mwana, aliyeitwa Sauli, kijana, tena mzuri; wala katika wana wa Israeli hakuwako mtu mzuri kuliko yeye; tangu mabega yake kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wote.
1 Samweli 10 : 23
23 Basi wakaenda mbio wakamleta kutoka huko; naye aliposimama kati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu wote, tangu mabega yake kwenda juu.
1 Samweli 11 : 15
15 Nao watu wote wakaenda Gilgali; wakamtawaza Sauli mbele za BWANA huko Gilgali; wakachinja sadaka za amani mbele za BWANA; na huko Sauli na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.
Hosea 13 : 11
11 Nimekupa mfalme katika hasira yangu, nikamwondoa katika ghadhabu yangu.
1 Samweli 14 : 2
2 Naye Sauli alikuwa akikaa katika Viunga vya Gibea, chini ya mkomamanga uliokuwa kwenye uwanja huko Migroni; na hao watu waliokuwa pamoja naye walikuwa watu mia sita;
1 Samweli 15 : 34
34 Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli.
Isaya 10 : 29
29 wamevuka kivuko; wamekwenda kulala katika Geba; Rama unatetemeka; Gibea wa Sauli umekimbia.
1 Samweli 14 : 46
46 Ndipo Sauli akakwea kuacha kuwafuata Wafilisti; nao Wafilisti wakaenda zao kwao.
1 Samweli 14 : 52
52 ⑤ Tena, kulikuwa na vita kali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu yeyote aliyekuwa hodari, au mtu yeyote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.
1 Samweli 13 : 14
14 ⑰ Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile BWANA alilokuamuru.
Leave a Reply