Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Satir
Mambo ya Walawi 17 : 7
7 Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi.
2 Mambo ya Nyakati 11 : 15
15 naye akajiwekea makuhani wa mahali pa juu, na wa wale majini, na wa zile ndama alizozitengeneza.
Isaya 13 : 21
21 ⑩ Lakini huko watalala wanyama wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko.
Isaya 34 : 14
14 Na hayawani wa nyikani watakutana na mbwamwitu, na beberu anamwita mwenziwe; naam, babewatoto anakaa huko na kupata pahali pa kustarehe.
Leave a Reply