Biblia inasema nini kuhusu sarah – Mistari yote ya Biblia kuhusu sarah

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia sarah

Mwanzo 21 : 1 – 34
1 BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema.
2 Sara akapata mimba akamzalia Abrahamu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.
3 Abrahamu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia.
4 ① Abrahamu akamtahiri Isaka mwanawe, alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwamuru.
5 Naye Abrahamu alikuwa mtu wa miaka mia moja, alipozaliwa mwana wake Isaka.
6 ② Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami.
7 ③ Akasema, Ni nani angemwambia Abrahamu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.
8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Abrahamu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.
9 ④ Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Abrahamu, anafanya dhihaka.
10 ⑤ Kwa hiyo akamwambia Abrahamu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.
11 ⑥ Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Abrahamu, kwa ajili ya mwanawe.
12 ⑦ Mungu akamwambia Abrahamu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
13 ⑧ Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.
14 ⑩ Abrahamu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akamtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
15 ⑪ Yale maji yalipoisha katika kiriba, Hajiri akamlaza kijana kichakani.
16 ⑫ Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
17 ⑬ Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
18 ⑭ Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
19 ⑮ Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
20 ⑯ Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
21 ⑰ Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
22 ⑱ Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Abrahamu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda.
23 ⑲ Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake.
24 Abrahamu akasema, Nitaapa.
25 ⑳ Kisha Abrahamu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamemnyang’anya.
26 Abimeleki akasema, Mimi sijui ni nani aliyetenda neno hili, wala hukuniambia, wala sikusikia habari hii ila leo tu.
27 Abrahamu akatwaa kondoo na ng’ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano.
28 Abrahamu akawaweka wana-kondoo saba wa kike peke yao.
29 Abimeleki akamwuliza Abrahamu, Hawa wana-kondoo saba majike, uliowaweka, maana yake ni nini?
30 Akasema, Hawa wana-kondoo saba majike utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki.
31 Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili.
32 Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.
33 Abrahamu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.
34 Abrahamu akaishi kama mgeni kwa Wafilisti siku nyingi.

Mwanzo 16 : 15
15 ⑤ Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa.

Yohana 1 : 25
25 Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?

Yohana 1 : 19 – 25
19 Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?
20 Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.
21 Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.
22 Basi wakamwambia, U nani? Na tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wanenaje juu yako mwenyewe?
23 Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.
24 Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo.
25 Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *